• HABARI MPYA

    Thursday, July 10, 2014

    NI ARGENTINA NA UJERUMANI FAINALI KOMBE LA DUNIA 2014, UHOLANZI YAFIA KWENYE MATUTA

    ARGENTINA imetinga fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuifunga Uholanzi kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 Uwanja wa Sao Paulo nchini Brazil.
    Sifa zimuendee kipa Sergio Romero aliyeokoa penalti mbili za Ron Vlaar na Wesley Sneijder na kuipeleka Argentina Fainali.
    Arjen Robben na Dirk Kuyt pekee ndiyo walifunga penalti upande wa Uholanzi, wakati za Argentina zilikwamisha kimiani na Maxi Rodriguez, Sergio Aguero, Ezequiel Garay na Lionel Messi.
    Lionel Messi alifunga penali ya kwanza Argentina

    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Cuneyt Cakir wa Uturuki, timu zote zilishambuliana kwa zamu na sifa ziwaendee walinzi na makipa wa timu hizo waliofanya kazi ya ziada kulinda nyavu.
    Arjen Robben alikuwa mwiba mbele ya safu ya ulinzi ya Argentina- kadhalika na Lionel Messi alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Uholanzi katika mchezo huo wa marudio ya fainali ya mwaka 1978.   Shoot-out hero: Sergio Romero saves Ron Vlaar's penalty as Argentina prevailed 4-2 in the shoot-out to reach the final
    Shujaa wa matuta: Sergio Romero akiokoa penalti ya Ron Vlaar

    Argentina sasa itamenyana na Ujerumani katika fainali ambayo jana iliwatoa wenyeji Brazil kwa mabao 7-1.
    Kikosi cha Uholanzi kilikuwa: Cillessen, De Vrij, Vlaar, Martins Indi/Janmaat dk46, Kuyt, De Jong/Clasie dk62, Sneijder, Wijnaldum, Blind, Robben na Van Persie/Huntelaar dk96.
    Argentina: Romero, Zabaleta, Demichelis, Garay, Rojo, Biglia, Mascherano, Lavezzi/Maxi Rodriguez dk101, Messi, Perez/Palacio dk81 na Higuain/Aguero dk82.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI ARGENTINA NA UJERUMANI FAINALI KOMBE LA DUNIA 2014, UHOLANZI YAFIA KWENYE MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top