• HABARI MPYA

    Friday, July 04, 2014

    MARADONA ASEMA; "ARGENTINA HAICHEZI KITIMU, INAMTEGEMEA MESSI TU"

    TIMU ya Argentina inacheza chini ya kiwango chake na zaidi inamtegemea Lionel Messi- na kama wanataka kuifunga Ubelgiji katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Dunia, lazima wabadilke, amesema Diego Maradona.
    "Bado hatujalianzisha," amesema Maradona, ambaye alishinda Kombe la Dunia mwaka 1986 akiwa na Argentina, wakati akiizungumzia ushiriki wa timu hiyo katika fainali za mwaka huu nchini Brazil.
    "Wanatakiwa kuweka vichwani mwao hilo, hatuwezi kuwa tunamtegemea Messi. Labda anaweza kufunga bao zuri... lakini kama hatutabadilika kesho (leo), kwa kumtegemea yeye tu itakuwa ngumu sana kuvuka,".

    Tegemeo: Diego Maradona anaamini Argentina inamtegemea Lionel Messi katika Kombe la Dunia
    In the know: Maradona, pictured here with Gary Lineker, says they are in danger of becoming 'Sporting Messi'
    Maradona akiwa gwiji mwenzake, Gary Lineker 

    Maradona, aliyekuwa kocha wa Argentina katika fainali zilizopita za Kombe la Dunia ambazo walitolewa katika Robo Fainali, alisema hayo wakatr akizungumza na Televisheni ya Venezuelan baada ya Argentina kuifunga Uswisi wiki hii. Taarifa yake iliripotiwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya Habari vya Habari vya  Latin American jana.
    Amesema Argentina yenye jina kubwa imekuwa ikicheza kwa asilimia 40 tu na akawakandia kwa kupata ushindi mbwembamba wa 1-0 dhidi ya Uswisi tena kwa bao la dakika ya mwisho kwenye dakika za nyongeza.
    "Mtu kwa mtu, na kwa ujumla, Argentina ni wazuri. Wao (Uswisi) wanacheza kwa umakini, lakini wana wanasoka bora wachache," amesema Maradona mtata wakati wote.
    Argentina, ambayo ilifanya mazoezi ya kujifungia milango jana mjini Belo Horizonte kabla ya kwenda Brasilia kwa ajili ya mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Ubelgiji.
    Messi ameshinda uchezaji bora katika mechi tatu za kundi lao na kufunga mabao manne kati ya sabaza Argentina hadi sasa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MARADONA ASEMA; "ARGENTINA HAICHEZI KITIMU, INAMTEGEMEA MESSI TU" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top