Mwana ukome: Wachezaji wa Ujerumani wakishangilia ushindi wao wa 7-1 dhidi ya Brazil katika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia usiku huu

Lawama: Wachezaji wa Brazil, kutoka kushoto Fernandinho, Maicon na David Luiz

La kwanza: Thomas Muller akiifungia Ujerumani bao la kwanza

Kipa Julio Cesar akishindwa kuzuia shut la Thomas Muller, huku David Luiz akiangalia

Mvunja rekodi: Miroslav Klose akishangilia baada ya kuibuka mfungaji bora wa kihistoria wa Kombe la Dunia

Klose amevunja rekodi ya gwiji wa Brazil, Ronaldo akifunga mabao mawili leo

Klose akifunga huku kiungo wa Fernandinho akimsindikiza kwa macho

Kroos akiondoka kushangilia baada ya kufunga

Sammy Khedira akiifungia Ujerumani bao la tano

Ujerumani wakipongezana huku, wachezaji wa Brazil wakitawanyika Uwanja wa Mineirao

Beki wa Brazil, David Luiz akienda chini wakati anakabiliana na Miroslav Klose

Sami Khedira akimtoka Luis Gustavo wa Brazil

Beki wa Ujerumani, Mats Hummels akimzuia Fred huku Oscar akiwa tayari kutoa msaada

Beki wa Ujerumani, Jerome Boateng akizinguana na Marcelo wa Brazil



.png)
0 comments:
Post a Comment