BEKI David Luiz amesema atamudu presha ya kuiongoza nchi hiyo yenye watu Milioni 200, wakati Brazil itakapomenyana na Ujerumani kesho katika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia.
Beki huyo wa zamani wa Chelsea atakuwa Nahodha wa timu yake kesho, kufuatia FIFA kuipilia mbali rufaa ya Thiago Silva kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwenye michuano ya mwaka huu katika mchezo dhidi ya Colombia ambao timu yake ilishinda 2-1.
Nyota kinda wa Brazil, Neymar pia ataikosa Nusu Fainali kwa sababu ni majeruhi, lakini Luiz anaamini watatinga Fainali itakayochezwa Jumappili Uwanja wa Maracana.
Beki huyo wa kati wa Paris St Germain amesema: "Niko tayari. Mimi Nahodha Msaidizi na kundi hili ni rahisi saran kulimudu kwa sababu kila mmoja ni mtaratibu. Haitakuwa kazi ngumu kabisa,".
Big Phil: Kocha Scolari akitoa maelekezo kwa vijana wake mazoezini mjini Teresopolis
Luiz akimuonyesha kitu Marcelo



.png)
0 comments:
Post a Comment