Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) imeiondoa Equatorial Guinea kwenye mechi za kufuzu kwa ajili ya fainali hizo zitakazofanyika nchini Morocco 2015.
Taarifa ya CAF iliyotumwa BIN ZUBEIRY leo imesema kwamba, uamuzi huo umetolewa jana, kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Soka Mauritania baada ya Raundi ya kwanza katika mchezo wa Mei 17, 2014 baina yao na Equatorial Guinea mjini Nouakchott.
Mauritania ilituma malalamiko dhidi ya mchezaji Thierry Fidieu Tazemeta, mwenye asili ya Cameroon, aliyezaliwa Oktoba 13, mwaka 1982 mjini Mbouda, kwa mujibu maelezo yaliyowasilishwa na Shirikisho la Soka la Cameroon.
Kamati imeamua kwamba mchezaji huyo aliamua kubadili uraia, lakini Shirikisho la Soka la Equatorial Guinea halikuwasilisha ushahidi kwamba mchezaji huyo alikuwa halali kuiwakilisha nchi hiyo kwa mujibu wa kanuni za FIFA.
Hakuna hati ya maandishi iliyowasilishwa inayoonyesha FIFA iliridhia ubadilishwaji wa uwakilishi wa mataifa wa mchezaji huyo.
Kwa sababu hiyo, Mauritania imefuzu kwa Raundi ya Pili ya mchujo wa AFCON 2015 na sasa itamenyana na Uganda katika hatua hiyo ya mwisho ya mchujo mchezo wa kwanza ukichezwa Julai 19 mjini Kampala.

![]() |
| Emmanuel Okwi wa Uganda kulia, sasa timu yake itamenyana na Mauritania kuwania kufuzu AFCON 2015 |
Mauritania ilituma malalamiko dhidi ya mchezaji Thierry Fidieu Tazemeta, mwenye asili ya Cameroon, aliyezaliwa Oktoba 13, mwaka 1982 mjini Mbouda, kwa mujibu maelezo yaliyowasilishwa na Shirikisho la Soka la Cameroon.
Kamati imeamua kwamba mchezaji huyo aliamua kubadili uraia, lakini Shirikisho la Soka la Equatorial Guinea halikuwasilisha ushahidi kwamba mchezaji huyo alikuwa halali kuiwakilisha nchi hiyo kwa mujibu wa kanuni za FIFA.
Hakuna hati ya maandishi iliyowasilishwa inayoonyesha FIFA iliridhia ubadilishwaji wa uwakilishi wa mataifa wa mchezaji huyo.
Kwa sababu hiyo, Mauritania imefuzu kwa Raundi ya Pili ya mchujo wa AFCON 2015 na sasa itamenyana na Uganda katika hatua hiyo ya mwisho ya mchujo mchezo wa kwanza ukichezwa Julai 19 mjini Kampala.

.png)
0 comments:
Post a Comment