JOSEPH Marius Omog ni kocha ambaye Desemba mwaka huu atatimiza mwaka mmoja tangu ajiunge na Azam FC, akitokea Leopard FC ya Kongo Brazaville.
Akitoka kuipa mafanikio timu hiyo ya Kongo ikiwemo kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF), Mcameroon huyo aliipa na Azam FC ubingwa wa Bara Mei mwaka huu.
Lakini siku chache baada ya kuanza kazi, Omog alikasirishwa na kukatishwa tamaa na hali halisi ya timu, akasema anahitaji kuiboresha mno, kwani wachezaji wengi waliokuwapo hawana ubora.
Hayo yalifuatia Azam FC kutolewa katika Raundi ya Awali tu ya Kombe la Shirikisho Afrika na Ferroviario ya Msumbiji.
Hata hivyo, Omog akatulia na kujipanga upya, akiwatumia wachezaji wengi zaidi wa akademi katika mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu hadi kutwaa ubingwa.
Ni ukweli, ubora wa Azam msimu waliomaliza na ubingwa ulishuka mno ukilinganisha na msimu uliotangulia ambao walimaliza nyuma ya Yanga nafasi ya pili.
Baada ya msimu, Omog aliwatema wachezaji kadhaa wakiwemo Malika Ndeule, Luckson Kakolaki, Jabir Aziz, Samih Haji Nuhu, Ibrahim Mwaipopo na Ismail Kone kutoka Ivory Coast.
Baada ya hapo, zoezi la kusajili wapya lilichukua nafasi yake na miongoni mwa waliosajiliwa ni wachezaji waliomaliza mikataba Yanga, kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu.
Awali ya hapo, hata kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu, iliripotiwa mchezaji kutoka Mali, Ismaila Diara alikuja kufanya majaribio na akafuzu na kupewa Mkataba.
Hivyo naye kambi ya kujiandaa na msimu ujao ilipoanza akawasili na hadi sasa anaendelea na mazoezi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Bahati mbaya, Azam wakagundua kiungo Frank Domayo ni majeruhi na hataweza kucheza hadi mwakani baada ya kufanyiwa upasuaji, hivyo wakajikuta wanahitaji kusajili kiungo mwingine.
Kwa haraka haraka, wazo la viongozi ambao wapo karibu na timu likawapeleka kwa mchezaji mwingine aliyemaliza Mkataba wake Yanga SC, Athumani Iddi ‘Chuji’.
Chuji akaitwa mazoezini Azam FC na katika siku ya kwanza tu ya kufanya mazoezi Chamazi, kocha Omog akamkubali akasema kwa uzoefu wake ataisaidia timu.
Lakini wakiwa ofisini wameketi, viongozi wakuu wa Azam wakasikia Chuji amefanya mazoezi Chamazi, inadaiwa walikasirika na kutoa agizo aondolewe mara moja, wakidai ni mtovu wa nidhamu.
Wakati hiyo ikiwa hukumu ya Chuji, mchezaji mwingine naye, Diara kutoka Mali ameanza kupigwa mizengwe- anaambiwa hajui hata kupiga danadana hafai.
Sasa hivi mchezaji anayesifiwa ni mshambuliaji Leonel Saint-Preux kutoka Haiti na maana yake sasa, huyo anapigiwa debe achukue nafasi ya Diara.
Diara kasainishwa Mkataba na kachukua fedha za Azam za kusaini na pia akivunjiwa Mkataba atalipwa. Tayari Azam ilimlipa Kone ili kuvunja Mkataba wake wakati pia alipewa fedha za usajili.
Mganda Brian Umony hatima yake haieleweki hadi sasa, kama atabaki au ataachwa. Lakini naye kama ataachwa, ina maana atalipwa kwa sababu bado ana mkataba.
Inataka kuwa kama desturi ndani ya Azam, kutojali kuwa makini kabla ya kumsainisha mchezaji kwa sababu tu; “akionenaka hafai atalipwa aondoke”.
Makocha wamekuwa wakilipwa na kuondoka baada ya kuvunjiwa mikataba- na wachezaji kadhalika.
Inapotokea mara moja au mara mbili, ni bahati mbaya, lakini kwa Azam sasa linataka kuwa jambo la kawaida.
Hii maana yake kuna watu hawatekelezi majukumu yao ipasavyo, ama wanakosa uhuru wa kutosha wa kutekeleza majukumu yao, au hawawezeshwi.
Haiwezi mchezaji afike majaribio, apitishwe halafu baada ya muda aambiwe hajui hata kupiga danadana. Hiyo ni fedheha.
Leo imetokea dharula ya Domayo kuumia, wakati klabu imeacha viungo wengi kwa ushauri wa mwalimu Omog, watu wa benchi la Ufundi wakapendekeza Chuji achukuliwe kwa mkataba wa muda mfupi kuziba pengo, lakini viongozi wa juu wanapinga.
Maana yake hapo watu wameingiliwa katika majukumu yao na kesho likitokea tatizo, tayari wana utetezi.
Ndiyo, watasema walijua mapema wakapendekeza Chuji asajiliwe, lakini akakataliwa.
Azam lazima ijitofautishe na klabu kongwe nchini zinazoendeshwa kimizengwe siku zote, kwa kukubali kuufuata mfumo wa mgawanyo majukumu na kuheshimu watu iliyowapa majukumu.
Ndani ya Azam, lazima kila mmoja awe tayari kuunga mkono juhudi za mwenzake katika timu na si kuleta mambo ya kibinafasi, kila mtu anataka jambo zuri liwe lile lilipotia mikononi mwake. Hapana.
Azam ni klabu ndogo ambayo haifai kuwa na makundi, badala yake iwe na umoja wa nguvu.
Watu wawe tayari kuunga mkono jitihada za wengine, na si kuleteana upinzani usio na kichwa wala miguu. Tazama kama sasa, mchezaji leo anasajiliwa kesho anatimuliwa, analetwa mwingine, mambo kama haya wakati fulani Simba na Yanga zilikuwa zinajikuta zinaacha wachezaji wazuri zinakwenda kusajili magalasa. Ndiyo, ile wahenga wanasema, kuchamba kwingi, mwisho utashika kinyesi. Ramadhan karim.

.png)
0 comments:
Post a Comment