• HABARI MPYA

    Tuesday, September 03, 2013

    MAZEMBE YAWAZUIA SAMATTA NA ULIMWENGU KUJA STARS KUKAMILISHA RATIBA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA SEPTEMBA 3, 2013, SAA  11:52 JIONI
    KLABU ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imezuia washambuliaji wake Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu kuja kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Syars.
    Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema anaipa umuhimu mkubwa mechi ya mwisho ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia kwa lengo ni kuhakikisha wanamaliza wakiwa wa pili katika kundi hilo na kwa sababu hiyo kuwakosa wawili hao ni pigo kwake.
    Mazembe imetuma taarifa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo mchana ikidai ni wawili hao ni wagonjwa- lakini ukweli ni kwamba inataka iwatumie kwenye mechi za makundi za Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
    Samatta na Ulimwengu wamekuwa tegemeo la mabao Taifa Stars siku za karibuni

    Mechi hiyo itachezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul, Gambia ambapo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premiem Lager itaondoka kesho (Septemba 4 mwaka huu) saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Dakar, Senegal.
    Kim amesema wanataka kushinda ugenini, kwani licha ya kuwa wameshatolewa lakini ushindi utawaongezea pointi kwa ajili ya viwango (rankings) vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na pia kuepuka kuanzia ngazi ya awali ya mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa fainali za 2015.
    “Tunacheza mechi hii tukiwa katika mazingira magumu, kwani wengi wa wachezaji wa kikosi cha kwanza ni majeruhi. Sijawahi kukutana na hali hii tangu nilipoanza kuifundisha Taifa Stars, lakini tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri,” amesema Kim.
    Amesema kwa mipango ya timu yake mechi hiyo ni muhimu tofauti na wengi wanavyofikiria, na uamuzi wake wa kumwita beki Henry Joseph amezingatia mambo mengi ya kiufundi ikiwemo nafasi anayocheza na uzoefu wa mchezaji aliyekuwa akicheza nchini Norway katika klabu ya Kongsvinger IL.
    Wachezaji majeruhi katika kikosi hicho ni Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Salum Abubakar, Athuman Idd na John Bocco.
    Wachezaji wanaoondoka kwenda Banjul ni Juma Kaseja, Mwadini Ali, Ali Mustafa, Amri Kiemba, David Luhende, David Mwantika, Erasto Nyoni, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Henry Joseph, Jonas Mkude, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Said Dilunga, Simon Msuva na Vincent Barnabas.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAZEMBE YAWAZUIA SAMATTA NA ULIMWENGU KUJA STARS KUKAMILISHA RATIBA KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top