• HABARI MPYA

    Tuesday, August 13, 2013

    TAIFA STARS LA KUVUNDA, AU?

    Na Mahmoud Zubeiry, Soweto, Afrika Kusini
    IMEWEKWA AGOSTI 13, 2013 SAA 11:46 ALFAJIRI
    KABLA ya mwaka 2006, hali ilikuwa mbaya juu ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kutokana na kutokuwa mdhamini wala utaratibu maalum kuhusu makocha.
    Ni katika kipindi hicho ilishuhudiwa wachezaji wakiwa hawafurahii kuchezea timu ya nchi yao- kutokana na hali mbaya kwa ujumla. Kukaa katika kambi isiyo na hadhi pale Jeshi la Wokovu, huduma mbovu na posho duni, ambazo pia walikuwa wanakopwa.
    Bado viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) tangu enzi za FAT walifanya jitihada za kuunda Kamati za kusimamia timu, zikihusisha wadau mbalimbali wa soka, wengi wao wafanyabiashara maarufu kama Reginald Mengi, Azim Dewji na Mohamed Dewji.
    Mambo yalibadilika mwaka 2006, baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuamua kuisaidia timu hiyo na pia kuhamasisha Watanzania kuiunga mkono.
    Rais Kikwete aliamua kubeba jukumu la ajira za makocha wa kigeni na tangu mwaka 2006 timu hiyo imekwishapitia mikononi mwa walimu watatu wa kigeni, kuanzia Mbrazil, Marcio Maximo na Wadenmark, Jan Poulsen na sasa Kim Poulsen.   
    Pamoja na hayo, kwa miaka nane sasa Tanzania imeshindwa kutimiza ndoto za kushiriki tena Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, ikikosa Fainali nne kuanzia za Ghana 2008, Angola 2010, Gabon na  Equatorial Guinea 2012 na mwaka huu Afrika Kusini.
    Bado hadithi zi zile zile kila siku, wachezaji wetu hawana viwango vya kushindana kimataifa, pamoja na kwamba walimu wa timu za taifa wamekuwa wakipewa fursa nzuri za maandalizi.
    Maximo alipewa kambi mbili za nje ya nchi, Brazil na Ulaya, lakini akaambulia tu kuipeleka timu katika fainali za Ubingwa wa Mataifa Afrika (CHAN), zilizofanyika kwa mara ya kwanza Ivory Coast mwaka 2009. 
    Tangu mwaka 2006, Taifa Stars imekuwa na mdhamini wa kudumu, kuanzia Kampuni ya Bia ya Serengti (SBL) kwa pamoja na benki ya NMB, na sasa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
    Wachezaji wanapewa posho nzuri wanapokuwa kambini na bado Kamati ya Kusaidia timu hiyo nayo imekuwa ikiwapa bakhshishi nzuri hata wanapopoteza michezo, lakini bado matokeo mazuri limekuwa suala gumu. Tatizo nini?
    Stars enzi za Maximo

    STARS CHINI YA MAXIMO
    KATI ya Juni mwaka 2006 hadi Juni 2010, Taifa Stars ilikuwa chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo na katia kipindi hicho ilifuzu kucheza Fainali za kwanza za CHAN zilizofanyika Ivory Coast. 
    Huyu ni mwalimu kwanza wa kigeni Taifa Stars tangu kuondoka kwa Mjerumani Burkhad Pape mwaka 2002. 

    REKODI YA MAXIMO STARS
                   P W D L GF GA GD Pts
    Tanzania 44 16 15 13 53 48 5 63

    REKODI YA MARCIO MAXIMO TAIFA STARS:
    02/09/2006: Tanzania 2-1  Burkina Faso (Kufuzu AFCON) 
    30/09/2006:  Tanzania 0-0 Kenya (Kirafiki)
    08/10/2006: Msumbiji 0-0 Tanzania (Kufuzu AFCON) 
    18/11/2006: Tanzania 1-1  Angola (Kirafiki) 
    09/12/2006: Tanzania 2-0  DRC (Kirafiki)
    24/03/2007: Senegal 4-0  Tanzania (Kufuzu AFCON)
    26/05/2007: Uganda 1-1  Tanzania (Kirafiki) 
    02/06/2007: Tanzania 1-1  Senegal (Kufuzu AFCON) 
    09/06/2007: Tanzania 1-1  Zambia (Kirafiki) 
    16/06/2007: Burkina Faso 0-1 Tanzania (Kufuzu AFCON)
    01/09/2007: Tanzania 1-0  Uganda (Ufunguzi Uwanja wa Taifa) 
    08/09/2007: Tanzania 0-1  Msumbiji (Kufuzu AFCON)
    04/04/2008: Yemen 2-1  Tanzania (Kirafiki) 
    25/05/2008: Tanzania 1-1  Malawi (Kirafiki) 
    31/05/2008: Tanzania 1-1  Mauritius (Kufuzu Kombe la Dunia) 
    07/06/2008: Cape Verde  1-0  Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
    14/06/2008: Tanzania 0-0 Cameroon (Kufuzu Kombe la Dunia) 
    21/06/2008: Cameroon 2-1  Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
    20/08/2008: Tanzania 1-1  Ghana (Kirafiki) 
    06/09/2008: Mauritius 1-4   Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
    11/10/2008: Tanzania 3-1  Cape Verde (Kufuzu Kombe la Dunia)  
    19/11/2008: Tanzania 1-0 Msumbiji (Kirafiki) 
    11/02/2009: Tanzania 0-0 Zimbabwe (Kirafiki) 
    KUFUZU CHAN;
    Kenya 1-2  Tanzania
    Tanzania 1-0 Kenya 
    Tanzania 2-0 Uganda
    Tanzania 1-1  Uganda
    Tanzania 3-1  Sudan
    Sudan 1-2 Tanzania
    22/2/2009: Senegal 1 – 0  Tanzania (CHAN)
    25/2/2009: Tanzania 1 – 0 Ivory Coast (CHAN)
    28/2/2009: Zambia 1 – 1 Tanzania (CHAN)
    09/05/2009: Tanzania 0-2 DRC (Kirafiki) 
    03/06/2009: Tanzania 2-1 New Zealand (Kirafiki) 
    12/08/2009: Rwanda 1-2  Tanzania (Kirafiki) 
    05/11/2009: Misri 5-1 Tanzania (Kirafiki) 
    08/11/2009: Yemen 1-1  Tanzania (Kirafiki) 
    11/11/2009: Yemen 2-1  Tanzania (Kirafiki) 
    04/01/2010: Tanzania 0-1  Ivory Coast (Kirafiki) 
    03/03/2010: Tanzania 2-3 Uganda (Kirafiki)
    KUFUZU CHAN; 
    27/03/2010: Somalia 0-6 Tanzania
    01/05/2010: Tanzania 1–1 Rwanda
    06/06/2010: Rwanda 1–0 Tanzania
    07/06/2010: Tanzania 1-5 Brazil (Kirafiki)

    STARS CHINI YA JAN POULSEN
    KATI ya Julai mwaka 2010 hadi Mei 2012, timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilikuwa chini ya kocha Mdenmark, Jan Borge Poulsen na katika kipindi hicho haikufuzu kucheza Fainali zozote za michuano ya Afrika. 
    Lakini Pouseln akiwa na timu ya Bara, Kilimanjaro Stars aliiwezesha kutwaa Kombe la CECAFA Challenge mwaka 2010 mjini Dar es Salaam. 
    Jan Poulsen

    REKODI YA JAN POULSEN STARS
                    P W D L GF GA GD Pts
    Tanzania 22 5 7 10 16 28 -12 22

    REKODI YA JAN POULSEN TAIFA STARS
    11/08/2010: Tanzania 1-1 Kenya (Kirafiki) 
    03/09/2010: Algeria 1-1 Tanzania (Kufuzu AFCON) 
    09/10/2010: Tanzania 0-1  Morocco (Kufuzu AFCON) 
    05/01/2011: Misri 5-1  Tanzania (Kombe la Mafuta) 
    08/01/2011: Tanzania 1-1 Burundi (Kombe la Mafuta) 
    11/01/2011: Uganda 1-1 Tanzania (Kombe la Mafuta) 
    16/01/2011: Tanzania 0-2  Sudan (Kombe la Mafuta) 
    09/02/2011: Tanzania 1-0 Palestina (Kirafiki) 
    26/03/2011: Tanzania 2-1  Jamhuri ya Afrika ya Kati (Kufuzu AFCON)
    23/04/2011: Msumbiji  2-0 Tanzania (Kirafiki) 
    14/05/2011: Tanzania 0-1  Afrika Kusini (Kirafiki) 
    05/06/2011: Jamhuri ya Afrika ya Kati 2-1 Tanzania (Kufuzu AFCON)
    03/09/2011: Tanzania 1-1 Algeria (Kufuzu AFCON) 
    09/10/2011: Morocco 3-1 Tanzania (Kufuzu AFCON) 
    11/11/2011: Chad 1-2  Tanzania (Kufuzu AFCON)
    15/11/2011: Tanzania 0-1 Chad (Kufuzu AFCON)
    26/11/2011: Tanzania 0-1  Rwanda (Kirafiki) 
    29/11/2011: Tanzania 3-0 Djibouti (Kufuzu AFCON) 
    03/12/2011: Tanzania 1-2  Zimbabwe (Kirafiki) 
    06/12/2011: Tanzania 1-0 Malawi (Kirafiki) 
    23/02/2012; Tanzania 0-0 DRC (Kirafiki) 
    29/02/2012 Tanzania 1-1 Msumbiji (Kufuzu AFCON)

    Kuanzia Mei mwaka jana, Stars imehamia mikononi mwa Mdenmark mwingine, Kim Pouslen ambaye alishindwa kuiwezesha timu kucheza Fainali za mwaka huu za Mataifa ya Afrika, ikitolewa na Msumbiji.
    Ikiwa imebakiza mechi moja katika kundi lake, D kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil, tayari Stars imekwishatolewa na itacheza na Gambia kukamilisha ratiba tu.
    Baada ya kutolewa na Uganda katika kampeni za kuwania tiketi ya kucheza CHAN mwakani Afrika Kusini, Pouslen alizungumza katika hali fulani ya kukatishwa tamaa, ingawa anajipa moyo.
    Poulsen alisema kwamba imemsikitisha sana kutolewa CHAN, lakini sasa anajipanga upya kurejesha makali ya timu.
    Stars ilifungwa mabao 3-1 jana na Uganda Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala na kufanya kipigo cha jumla cha 4-1 baada ya awali kufungwa 1-0 Dar es Salaam na kuwapa The Cranes, Korongo wa Kampala, tiketi ya kwenda Afrika Kusini kwenye CHAN mwakani.
    Alisema kwamba kutolewa CHAN si mwisho na wamejifunza kutokana na makosa, yeye pamoja na wachezaji wake- na sasa wanajipanga upya kuendelea na safari.
    “Mimi na wachezaji tumesikitishwa kutolewa kwenye CHAN, ulikuwa mchezo mgumu nimesikitishwa, tumeanza kinyonge, baada ya dakika 10 tukafungwa 1-0, baada ya hapo nafikiri tumeona tulijiandaa vizuri kwa huu mchezo, tulianza kucheza vizuri, tukafunga ikawa 1-1,”.
    “Na Ngassa akagongesha mwamba kwa shuti la ajabu na kabla ya mapumziko, Frank Domayo akaumia. Na hii ilikuwa pigo kwa timu kwa sababu huu umekuwa muendelezo wa mwezi mgumu kwetu, tunakosa wachezaji fulani, na sasa ikatubidi tumkose mwingine mmoja,”.
    “Lakini pamoja na yote, kipindi cha pili tulimiliki vizuri mpira, tulihitaji bao moja tufuzu, lakini baada ya hapo, likaja pigo tena kwetu, ndani ya boksi kukiwa hakuna mtu, tukawapa wao penalti (David Luhende alinawa akiwa peke yake). Na unapofanya kosa kubwa kama hili, unajitengenezea ugumu,”.
    “Tukiwa nyuma kwa mabao 2-1, tukapata kona, wakaokoa kwenye mstari, ingekuwa 2-2. Na katika shambulizi hilo hilo, tukapoteza mpira kwa kosa kubwa, na wakafanya shambulizi la kushitukiza tukafungwa, ikawa 3-1,”.
    “Pia nikashangazwa sana, baada ya mchezo kuwa sisi tumefungwa 3-1, kisha marefa ndiyo wakabadilika na kuwa wazuri kwa Tanzania. Lakini kabla ya hapo, kila tukio la asilimia hamsini kwa hamsini, walipewa wenzetu. Hivyo nafikiri marefa walikuwa wachanga, ambao hawajakomaa kiasi cha kuumudu mchezo kama huu,”.
    Alipoulizwa kuhusu ahadi yake ya kuipeleka Stars fainali zijazo za Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuanza kazi Mei mwaka jana, Poulsen alisema kwamba amesikitishwa na kutolewa CHAN, lakini wanatakiwa kusimama imara na kuendelea na mapambano.
    “Tumekuwa katika kazi hii kwa miezi 14, mwanzoni tumecheza vizuri sana, hii ni mara ya kwanza ninaangushwa, kuangushwa haswa leo, lakini wakati huo huo, katika soka unatakiwa kuwa imara, kama unataka kushinda kila mchezo, ucheze vizuri,.”
    “Tumepoteza mchezo ambao tayari tulijitengenezea mazingira magumu katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam. Mimi ni aina ya watu hawa, na wachezaji ni wa aina hiyo pia, ukipoteza mechi, unajifundisha kutokana na makosa, kisha unasonga mbele,”.
    “Tuna malengo yetu, tunatakiwa kujizatiti, tunaweza kujizatiti na kusonga mbele, tunaweza kufanya na tutafanya. Nilikuambia, unapoanza safari inakuwa na kona, kunakuwa na vigingi barabarani. Hivi vilikuwa vigingi na kona. Ni pigo, tumesononeshwa kuwa nje ya CHAN, lakini si mwisho, tuko tayari kupambana upya,”alisema.
    Lakini bado wachezaji wenyewe wana mawazo tofauti na falsafa ya kocha kuhusu aina ya wachezaji wanaostahili kuitumikia timu hiyo.
    Kipa mkongwe na Nahodha timu hiyo, Juma Kaseja alisema baada ya timu kutolewa CHAN kwamba ipo haja mashabiki wa soka nchini kubadilisha mitazamo yao kwamba wachezaji chupikizi ndiyo wanaofaa kuliko wakongwe.
    Kaseja alisema kwamba mashabiki wamekuwa wakitaka sana wachezaji chipukizi wapewe nafasi, lakini ukweli ni kwamba hawamudu kazi.
    “Tusaidieni kuwaelimisha mashabiki, wao wanataka sana wachezaji chipukizi, lakini nadhani mmeona leo (Julai 27, 2013), hawawezi. Wanahitaji kupewa muda wakomae taratibu. Hata sisi tulipokuwa chipukizi, tulikomazwa taratibu,”alisema Kaseja.
    Ingawa Kaseja hakuweka wazi, lakini alikuwa anawazungumzia wachezaji chipukizi walivyoigharimu Stars kutolewa na Uganda CHAN.
    Beki chipukizi, David Luhende aliyeitwa Stars kwa mara ya kwanza safari hiyo, aliunawa mpira akiwa peke yake- baada ya kushindwa kuumiliki vyema na kusababisha penalti, wakati huo timu hizo zikiwa zimefungana 1-1 na Brian Majwega akaifungia Uganda bao la pili.
    Kiungo chipukizi, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyepandishwa timu hiyo Mei mwaka jana, alijaribu kuwapiga chenga wachezaji wawili wa Uganda, wakati huo wachezaji karibu wote wa Tanzania wamepanda kufuata shambulizi la kona, akapokonywa mpira na likafanywa shambulizi la kushitukiza, Stars ikafungwa bao la tatu.
    Wachezaji wengine chipukizi walioingizwa kipindi cha pili siku hiyo, Simon Msuva na Haroun Chanongo walishindwa kuisaidia timu kubadilisha matokeo japo kidogo siku hiyo.   
    Lakini pia uzalendo wa wachezaji, nalo linaonekana kuwa bado tatizo- kwani Kim alilalamimikia wachezaji kugoma kujiunga na timu kwa kutoa visingizio.
    Siku moja kabla ya Taifa Stars kushuka dimbani kumenyana na wenyeji, Uganda, The Cranes kuwania tiketi ya CHAN, BIN ZUBEIRY iligundua kocha Poulsen alilazimika kufanya kazi kubwa kuwashawishi wachezaji kadhaa nyota kujiunga na timu kwa ajili ya mechi hiyo.
    Wachezaji kadhaa nyota, wakiwemo viungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Athumani Iddi ‘Chuji’ na mshambuliaji, John Bocco ‘Adebayor’ hawakutaka kwenda hata Mwanza, ambako Stars iliweka kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo huo, baada ya kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza.
    Kocha Poulsen na Msaidizi wake, Sylvester Marsh waliwabembeleza mno wachezaji hao kupanda ndege kwenda Mwanza hadi wakakubali na kwa Bocco ilibidi apelekwe na Katibu wa klabu yake, Azam FC, Nassor Mohammed Idrisa ‘Father’ baada ya kugoma kabisa.
    Sure Boy alikuwa anakataa kwenda Mwanza kwa sababu anaumwa, wakati Chuji alikuwa anakataa kwa sababu ya kuwekwa benchi Stars na Bocco hakutaja sababu.
    Chuji alikuwa hatumiwi na Poulsen Stars licha ya kuitwa mara zote na alikaa benchi kwa dakika zote 90 Stars ikilala 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Uganda na baada ya mechi hiyo akasema anajitoa kwa sababu umuhimu wake hauonekani katika timu hiyo ya nchi.
    Lakini kutokana na kiungo Mwinyi Kazimoto kutimkia Qatar, Poulsen akalazimika kumbembeleza Chuji abaki kikosini.
    Hata wakati timu ikiwa Mwanza, wachezaji hao wote walikuwa wanataka kugoma kwenda Kampala na Poulsen na Marsh wakajitwisha jukumu lingine la kuwambeleza kupanda ndege kwenda Uganda.
    Thomas Ulimwengu Stars dhidi ya Ivory Coast

    Poulsen pia alisema kwamba amekuwa akiwaita mara kadhaa mabeki Wazanzibari, Nassor Masoud ‘Chollo’ na Waziri Salum, lakini wamekuwa wakitoa visingizio mara zote vya kuepuka kujiunga na timu hiyo.
    Poulsen alikuwa akizungumzia sababu ya kutokuwa na mabeki wengi wa pembeni katika kikosi chake, na pia muda mwingi akimchezesha kiungo Shomary Kapombe katika nafasi hiyo.
    Alisema kila mara anapomuita Chollo wa Simba SC na Waziri wa Azam FC, zote za Dar es Salaam wamekuwa wakitoa udhuru- maana yake hawataki kuchezea timu ya taifa, naye ameona hana sababu ya kuendelea kuwalazimisha.
    Alisema nafasi ya beki wa pembeni ni ngumu na anahitaji kumuandaa mchezaji yeyote kabla ya kuanza kumtumia, ila kwa sasa kutokana na dharula amelazimika kumchukua David Luhende.
    “Luhende akiwa anacheza Yanga anakuwa ana asilimia 60 ya kushambulia na 40 ya kuzuia. Sasa unapokuja timu ya taifa, inabadilika, kwa sababu unacheza mechi dhidi ya timu ngumu kama za Afrika Magharibi na kwingine katika nchi zilizoendelea. Huku (Stars) asilimia kubwa inakuwa kukaba,”alisema.
    “Huwezi kucheza dhidi ya mtu kama Gervinho au Solomon Kalou, halafu uwe unashambulia zaidi, lazima umdhibiti sana,”alisema.
    Lakini upande wa pili, wachezaji wa Stars nao wamekuwa wakimlalamikia kocha Poulsen kuwapa mazoezi magumu hadi siku moja kabla ya mechi, kwamba yanawaumiza wanashindwa kucheza vizuri.
    Mwinyi Kazimoto Stars na Uganda kufuzu CHAN

    Tunafahamu matatizo ya wachezaji wetu, hawapendi mazoezi magumu ambayo ndiyo humjenga mchezaji- lakini pia mazoezi magumu yanapotolewa katika mpangilio mbovu, kweli yanawaathiri wachezaji.
    Mechi 15 tu ndani ya mwaka mmoja na ushei, tayari Kim Pouslen anaelekea kufeli pia, nini tatizo haswa, au ndiyo kama walivyosema wahenga, la kuvunda halina ubani? Tujadili sasa.
    Kim Poulsen tayari maji ya shingo

    REKODI YA KIM POULSEN STARS
    P W D L GF GA GD Pts
    Tanzania 15 5 4 6 17 20 -3 19

    Mei 26, 2012
    Tanzania 0 – 0 Malawi (Kirafiki)
    Juni 2, 2012
    Ivory Coast 2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Juni 10, 2012
    Tanzania 2 – 1 Gambia (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Juni 17, 2012
    Msumbiji 1 – 1 Tanzania  (Tanzania ilitolewa kwa penalti kufuzu Mataifa ya Afrika)
    Agosti 15, 2012
    Botswana 3 – 3 Tanzania (Kirafiki)
    Novemba 14, 2012
    Tanzania 1-0 Kenya (Kirafiki)
    Desemba 22, 2012
    Tanzania 1-0 Zambia (Kirafiki)
    Januari 11, 2013
    Tanzania 1-2 Ethiopia (Kirafiki)
    Februari 6, 2013
    Tanzania 1-0 Cameroon (Kirafiki)
    Machi 24, 2013
    Tanzania 3-1 Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Juni 2, 2013
    Sudan 0 – 0 Tanzania (Mechi ya kirafiki Ethiopia)
    Juni 8, 2013 
    Morocco 2-1 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Juni 6, 2013 
    Tanzania 2-4 Ivory Coast (Kufuzu Kombe la Dunia)
    Julai 13, 2013
    Tanzania 0-1 Uganda (Kufuzu CHAN)
    Julai 27, 2013
    Uganda 3-1 Tanzania (Kufuzu CHAN)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TAIFA STARS LA KUVUNDA, AU? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top