Na Mahmoud Zubeiry, Soweto, Afrika Kusini
IMEWEKWA AGOSTI 13, 2013 SAA 11:48 ALFAJIRI
AZAM FC jana ilihitimisha ziara yake ya Afrika Kusini kwa kipigo cha bao 1-0 mbele ya wenyeji, Moroka Swallows kwenye Uwanja wa Volkswagen Dobsonville mjini Soweto- huo ukiwa mchezo wa tatu kufungwa hapa, baada ya awali kuchapwa 3-0 na Kaizer Chiefs, 2-1 na Orlando Pirates, wakati mchezo pekee iliyoshinda ni dhidi ya Mamelodi Sundowns 1-0. BIN ZUBEIRY imefanya mahojiano na kocha wa Azam, Muingereza Stewart John Hall juu ya ziara ya siku 12 ya timu hiyo nchini hapa kujiandaa na msimu. Endelea.
BIN ZUBEIRY: Mmemaliza kambi kwa matokeo ya kupoteza mechi tatu na kushinda moja, unaizungumziaje hii.
STEWART: Tungeweza kushinda leo, lakini tumepoteza nafasi nyingi, nimefurahishwa na kiwango cha timu, ingawa matokeo sijayapenda. Tumekuja hapa kuangalia kiwango cha timu si matokeo. Tumecheza vizuri mechi zote, nimefurahi.
BIN ZUBEIRY: Kwa ujumla, kambi ya Afrika Kusini unaielezeaje kwa mustakabali wa timu yako kuelekea msimu mpya.
STEWART: Hatukuja hapa kujiandaa kwa Ligi Kuu (ya Tanzania Bara) tu, tumekuja hapa kujiandaa na msimu kwa maana, pamoja na michuano ya Afrika pia. Tunaangalia mbali, kuanzia Ngao ya Jamii na Yanga Jumamosi, mechi ya kwanza ya Ligi na Mtibwa Sugar wiki ijayo. Tumekuja pia kujiandaa na Kombe la Shirikisho.
BIN ZUBEIRY: Unaanza na Yanga katika Ngao ya Jamii, hawa waliifunga Azam mechi zote msimu uliopita, unasemaje kuelekea mchezo huo
STEWART: Nilipokuwa hapa (Azam) kabla ya kuondoka, niliifunga Yanga mara nne msimu uliotangulia. 1-0, 2-0, 3-1, 3-0. Hatufikiri Yanga inatuzidi chochote, kwa sababu msimu uliotangulia tuliwafunga mara nne. Tuko tayari kuwafunga, tatizo kubwa unapocheza na Yanga ni marefa.
BIN ZUBEIRY: Kumbuka mwaka jana, ulipoteza mechi ya Ngao mbele ya Simba SC, je kwa Jumamosi matokeo yatabadilika?
STEWART: Sikuwapo wakati wa Ngao mwaka jana, sikuona huo mchezo. Siwezi kuuzungumzia.
BIN ZUBEIRY: Angalau Yanga watakuwa wanaongezewa nguvu na wachezaji wapya kadhaa, lakini kwako utawakosa Humphrey Meino na Brian Umony, unasemaje.
STEWART: Timu yangu iko sawa, Yanga wameongeza wachezaji kwa sababu labda wameona mapungufu.
BIN ZUBEIRY: Kwa ujumla nini matarajio yako katika Ligi Kuu, Yanga na Simba wanaonekana wako imara wote na ndiyo washindani wako wakuu
STEWART: Tuna bora zaidi yao, iliyokaa pamoja kwa muda wa kutosha, tunaweza kuwapiku katika mbio za ubingwa.
BIN ZUBEIRY: Kwa nini hukusajili majira haya ya joto
STEWART: Kwa sababu tuliamua, tuna akademi nzuri, na tumeamua kama tunatumia fedha nyingi katika akademi, hatuwezi kuendelea kusajili. Tunahitaji kupandiaha wachezaji. Nimepunguza kikosi cha kwanza hadi kubaki wachezaji 24, ili nipandishe watoto kutoka akademi.
BIN ZUBEIRY: Mwaka huu ulifikia hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho, unasemaje kuhusu mwakani
STEWART: Mwakani tunataka kufanya vizuri zaidi, kila mmoja alifurahia matokeo na kiwango chetu. Kwetu tulivutiwa na tunataka kufanya zaidi mwakani.
BIN ZUBEIRY: Baadhi ya wachezaji wa Azam wanaonekana dhahiri viwango vimeshuka hata mechi za kujipima nguvu hapa zimeonyesha, unasemaje juu ya hilo.
STEWART: Timu ya taifa ni tatizo kwetu, kwa mfano Mwadini Ally amekuwa akiitwa Taifa Stars kwa muda mrefu, lakini hachezi. Kuna kiwango cha mchezaji kufanya mazoezi, anatakiwa acheze. Tuna tatizo hilo pia kwa Vialli (Khamis Mcha). Erasto Nyoni naye amepoteza kujiamini kwa sababu amekuwa katika wakati mgumu Stars, leo amecheza vizuri. Vialli pia amecheza vizuri leo, hakufunga tu. Inaniumiza mchezaji anarejea kutoka Stars akiwa majeruhi, hatuambiwi. Sure Boy, Vialli na Bocco wote wamerudi majeruhi, na ndiyo maana wamshuka viwango, kwa sababu hawapo asilimia 100.
Nimefurahi kuwa na Paul Taylor ametusaidia katika tatizo la majeruhi. Ni mtaalamu wa tiba za wanamichezo.
BIN ZUBEIRY: Kipa Aishi Manula ameonekana kufanya vizuri zaidi ya Mwadini Ally katika mechi za hapa, hii kwa upande wako unaipokeaje
STEWART: Sote tunajua atakuwa kipa mzuri, atakwenda Sunderand kwa majaribio Novemba kwa wiki mbili, tukimalizia mzunguko wa kwanza wa Ligi, tunajua atakuwa kipa mzuri.
BIN ZUBEIRY: Atadaka mechi na Yanga?
STEWART: Atacheza, nataka kumpa uzoefu katika Uwanja mkubwa na mashabiki wengi. Tunajua ni kipa mzuri
BIN ZUBEIRY: Umepata Ratiba ya Ligi Kuu bila shaka, unaizungumziaje, inakutendea haki?
STEWART: Ratiba ni upumbavu mtupu. Tunacheza tarehe 24 na tarehe 28 mechi zote ugenini. Hii ni mbaya. Na tena kuna mapumziko ya kupisha kambi ya Stars kwa siku 14, taratibu za FIFA hazisemi hivyo, ni siku saba tu. Ligi inaumia kwa ajili hii. Tupo nje ya Kombe la Dunia Na CHAN. Kwa ni kambi yote hii?
BIN ZUBEIRY: Umekuwa ukilalamika sana misimu iliyopita kuonewa na marefa na bila shaka unaamini ilikukosesha ubingwa- una matarajio yoyote hali itabadilika?
STEWART: itakuwa vile vile.
BIN ZUBEIRY: Ina maana hakuna matumaini ya ubingwa Azam.
STEWART. Lazima tupambane kutimiza ndoto, tukijua marefa watakuwa si wazuri.
BIN ZUBEIRY: Inaonekana pia uhusiano wako na marefa wa Tanzania si mzuri, unadhani kwa nini?
STEWART: Nafikiri marefa wa Tanzania wanahitaji msaada. Kuongeza mishahara yao, posho zao na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kazi. Kama si hivyo wataendelea kupokea hongo na kuziumiza timu bora na kuzipendelea nyingine zinazowahonga.
BIN ZUBEIRY: Ulikuwa unamtumia Joackins Atudo katika beki ya kulia hapa Afrika Kusini, na msimu uliopita alikuwa anacheza katikati, maana yake unamhamisha?
STEWART: Kwa sababu tuna mabeki wa kati watano. Kumpeleka namba mbili, inatoa nafasi kwa watu zaidi kucheza. Atudo ameonyesha msimu uliopita ni beki mzuri wa kati. Na msimu huu mara nyingi atakuwa anacheza katikati.
BIN ZUBEIRY: Na kuna Erasto Nyoni katika beki ya kulia…
STEWART: Erasto anahuitaji kupumzika baada ya kucheza sana. Alikuwa ana wakati mbaya timu ya taifa, ameathirika kisaikolojia.
BIN ZUBEIRY: Na ni upi mustakabali wa Atudo kwa ujumla, ikiwa una mabeki wanne katikati zaidi yake, Aggrey Morris, Said Mourad, David Mwantika na Luckson Kakolaki.
STEWART: Atakuwa anacheza katikati mara nyingi
BIN ZUBEIRY: Umeweka kambi Afrika Kusini katika wakati wa baridi kali, unarejea Dar es Salaam kwenye joto kali, hii haitaleta athari kwa timu yako?
STEWART: Hapana, kwa sababu tunaenda nyumbani, tumezoea.
BIN ZUBEIRY: Himid Mao ulimtumia katika beki ya kulia msimu uliopita sasa unamrudisha nafasi yake ya kiungo, ambako pamesheheni, unasemaje.
STEWART: Mao ni mchezaji mzuri sana, ni muelewa. Tulimtumia katika beki ya kulia wakati ambao Erasto Nyoni alikuwa amesimamishwa, hatukuwa na beki. Ni mchezaji muhimu kwetu.
BIN ZUBEIRY: Ni ipi nafasi yake kwa sasa katika timu.
STEWART: Tutakapomuhtaji wakati wowote kucheza katika nafasi yoyote, atacheza popote kuisaidia timu.
BIN ZUBEIRY: Ina maana hana namba maalum.
STEWART: Ndiyo, ni kiraka
BIN ZUBEIRY: Gaudence Mwaikimba amekuwa akifunga mabao katika mechi za kujiandaa na msimu, lakini yanapokuja mashindano hachezi.
STEWART: Kwa kuwa sasa John Bocco hayupo vizuri kwa asilimia 100, Brian Umony ni majeruhi. Lazima tumuandae Mwaikimba. Ni vizuri kuwa na mchezaji wa akiba mzuri kama yeye. Ana historia nzuri ya kufunga na ni muhimu kwetu ndiyo maana tuko naye. Tena nina furaha kukuambia hakuna wakati ambao Mwaikimba yuko vizuri kama huu.
BIN ZUBEIRY: Kwa matatizo haya, maana yake ulitakiwa kusajili majira haya ya joto
STEWART: Hapana, sikuhitaji kusajili wakati bao bado ninao Vialli, Kipre Tchetche na Seif Abdallah.
BIN ZUBEIRY: Tumeona tatizo la ubifansi kwa washambuliaji wako katika mechi za hapa Afrika Kusini, kila mtu anataka kufunga kiasi cha kutojali hata kama mwenzake yupo katika nafasi nzuri zaidi.
STEWART: Ni kweli, tumelijadili hilo kwa mapana marefu, tumeambiana kweli, tumekubaliana kuacha ubinafsi na kuweka mbele maslahi ya timu
BIN ZUBEIRY: Hudhani kiu ya ufungaji bora inaleta haya. Maana misimu mitatu iliyopita, mfungaji bora Ligi Kuu anatoka Azam, kuanzia Mrisho Ngassa, John Bocco na sasa Kipre Tchetche.
STEWART: Haaa haa, kweli tangu niwe Azam imekuwa ikifunga mabao mengi na wafungaji bora ni wetu, hiyo ni kwa sababu tunacheza soka nzuri. Ila nataka nikuhakikishie hili ni tatzo la mpito.
BIN ZUBEIRY: Nashukuru kocha, naomba nikutakie usiku mwema, na safari njema.
STEWART: Asante sana, nashukuru pia kwa muda wako.

![]() |
| Stewart kushoto akiwa na Paul Talyor mjini Johannesburg |

| Azam One: Aishi Manula atadaka dhidi ya Yanga SC |

| Mwaikimba yuko sawa kuliko wakati wote kwa mujibu wa Stars |

| Taifa Stars imemshusha kiwango John Bocco |
BIN ZUBEIRY: Himid Mao ulimtumia katika beki ya kulia msimu uliopita sasa unamrudisha nafasi yake ya kiungo, ambako pamesheheni, unasemaje.
STEWART: Mao ni mchezaji mzuri sana, ni muelewa. Tulimtumia katika beki ya kulia wakati ambao Erasto Nyoni alikuwa amesimamishwa, hatukuwa na beki. Ni mchezaji muhimu kwetu.
BIN ZUBEIRY: Ni ipi nafasi yake kwa sasa katika timu.
STEWART: Tutakapomuhtaji wakati wowote kucheza katika nafasi yoyote, atacheza popote kuisaidia timu.
BIN ZUBEIRY: Ina maana hana namba maalum.
STEWART: Ndiyo, ni kiraka
BIN ZUBEIRY: Gaudence Mwaikimba amekuwa akifunga mabao katika mechi za kujiandaa na msimu, lakini yanapokuja mashindano hachezi.
STEWART: Kwa kuwa sasa John Bocco hayupo vizuri kwa asilimia 100, Brian Umony ni majeruhi. Lazima tumuandae Mwaikimba. Ni vizuri kuwa na mchezaji wa akiba mzuri kama yeye. Ana historia nzuri ya kufunga na ni muhimu kwetu ndiyo maana tuko naye. Tena nina furaha kukuambia hakuna wakati ambao Mwaikimba yuko vizuri kama huu.
BIN ZUBEIRY: Kwa matatizo haya, maana yake ulitakiwa kusajili majira haya ya joto
STEWART: Hapana, sikuhitaji kusajili wakati bao bado ninao Vialli, Kipre Tchetche na Seif Abdallah.
BIN ZUBEIRY: Tumeona tatizo la ubifansi kwa washambuliaji wako katika mechi za hapa Afrika Kusini, kila mtu anataka kufunga kiasi cha kutojali hata kama mwenzake yupo katika nafasi nzuri zaidi.
STEWART: Ni kweli, tumelijadili hilo kwa mapana marefu, tumeambiana kweli, tumekubaliana kuacha ubinafsi na kuweka mbele maslahi ya timu
![]() |
| Baridi kali; Stewart amesema baridi haitasumbua wairejea Dar es Salaam |

.png)