• HABARI MPYA

    Tuesday, August 13, 2013

    KILIMANJARO WAWAPA 'MARAHA' NYOTA SIMBA SC 'KIWANJA KIKUBWA'

    Na Ibrahim Kyaruzi, IMEWEKWA AGOSTI 13, 2013 SAA 3:11 ASUBUHI
    WADHAMINI wakuu wa klabu ya Simba, Bia ya Kilimanjaro, wanatarajia kufanya mambo makubwa zaidi kwa timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania, imefahamika.
    Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa semina maalumu iliyoandaliwa na wadhamini hao kwa ajili ya wachezaji, viongozi na benchi la ufundi la Simba iliyofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini.
    Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akizungumza katika semina hiyo

    “Kila mwaka Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiongeza thamani ya udhamini wake tangu tulipoanza mwaka 2008. Mwaka huu pia tutaleta kitu kingine kipya ambacho tutakitangaza wakati ukifika. Lengo ni kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika na udhamini huu,” alisema Kavishe. Kavishe aliongeza kuwa semina hiyo ilikuwa na lengo kuelezana masuala mbalimbali yanayohusiana na udhamini na jinsi ambavyo Simba SC na Kilimanjaro Premium Lager zinanufaika kutokana na udhamini huo na kuainisha maeneo ya kuboresha.
    Wachezaji Simba SC wakisikiliza


    Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdallah Kibadeni kulia akijadiliana na Msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo na Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang'are 'Kinesi' kushoto baada ya semina

    Beki Joseph Owino kulia na Abdulhalim Humud 'Gaucho' kushoto

    Joseph Owino kulia, Twaha Shekuwe 'Messi' na Abbel Dhaira kushoto

    Kibadeni na vijana wake

    Betram Mombeki kulia

    Kwa sasa, bia ya Kilimanjaro Premium Lager hutumia takribani Sh. Milioni 495 kwa ajili ya udhamini wake kwa klabu ya Simba kila mwaka, fedha ambazo hutumika kwa ajili ya ulipaji wa mishahara ya wachezaji, ukarabati wa majengo, kugharamia Mkutano Mkuu wa Wanachama, vifaa vya timu pamoja na tamasha Siku ya Simba.
    Akizungumza katika mkutano huo, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are, alisema semina hiyo imewafumbua macho viongozi na wachezaji katika masuala mbalimbali na kwamba kuanzia msimu ujao, klabu itajitahidi kufanya vizuri zaidi katika eneo la mahusiano bora na wadhamini pamoja na wadau wa klabu ya Simba.
    Kwa upande wa wachezaji, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, alisema semina hiyo imekuja katika wakati mwafaka kwa vile katika soka la sasa, udhamini na hadhi na maslahi ya wachezaji ni mambo yanayokwenda sambamba.
    Kilimanjaro Premium Lager imefanya semina hiyo kwa klabu ya Simba ili kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya mdhamini huyo na klabu na vile vile kuboresha. 
    Viongozi wa klabu ya Simba pamoja na benchi la ufundi na wachezaji ambao wengi ni wapya pia walitumia fursa hiyo kuweza kukaa pamoja katika mazingira mwanana na  tulivu kwenye hoteli hiyo ya kitalii huku wakishiriki michezo mbalimbali ya kujifurahisha ikiwemo mpira wa kikono, kuogelea na mingine kwa siku nzima. 
    Wadhamini hao wamepanga kufanya semina nyingine kama hiyo kwa ajili ya mabingwa wa ligi kuu, Yanga SC siku zijazo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KILIMANJARO WAWAPA 'MARAHA' NYOTA SIMBA SC 'KIWANJA KIKUBWA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top