IMEWEKWA AGOSTI 11, 2013 SAA 2:08 USIKU
MANCHESTER United imeweka jezi namba saba maalum kwa ajili ya Cristiano Ronaldo atakaporejea Old Trafford? David Moyes anajua.
MANCHESTER United imeweka jezi namba saba maalum kwa ajili ya Cristiano Ronaldo atakaporejea Old Trafford? David Moyes anajua.
Real Madrid imesema kwamba winga huyo wa zamani wa Manchester United hauzwi, na katika taarifa siyo rasmi, gazeti la kila siku la Hispania, Marca, hivi karibuni limetoa habari ukurasa wa mbele, ikisema ameongeza Mkataba mrefu wa kuendelea kupiga kazi Bernabeu.
Lakini hiyo haiwezi kumzuia Moyes kumuwekwa Ronaldo jezi yake aliyokuwa akivaa akiwa Manchester, namba saba (7) ikiwa haina jina wakati United ilipotambulisha kikosi chake cha msimu mpya.

Mwanzoni: Ronaldo alivaa jezi namba saba (7) kwa mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Bolton

Rio Ferdinand akishangilia na Ronaldo

Ronaldo aliifungia United bao la tatu katika fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Carling dhidi ya Wigan mwaka 2006
Antonio Valencia aliyekuwa anavaa jezi hiyo msimu uliopita sasa amehamia jezi namba 25.
Na ikiwa hajatajwa mtu mpya wa kuvaa jezi hiyo, ambayo awali ilipata umaarufu kupitia George Best, Moyes anaachwa maswali vichwani mwa mashabiki wa timu hiyo- kwamba huenda amemuachia Ronaldo aliyetimkia Madrid kwa dau la rekodi ya dunia.

Shujaa: Ronaldo alifanya vizuri enzi zake United

Ronaldo akishangilia bao na mchezaji mwenzake wa Ureno, Miguel Veloso

Nyota wa zamani wa United ameendelea kuvaa jezi namba saba (7) hata katika klabu yake ya sasa, Real Madrid


.png)