• HABARI MPYA

    Wednesday, August 14, 2013

    NGOMA INOGILE SAKATA LA SUAREZ, SASA AKANA KUSEMA ANATAKA KUBAKI LIVERPOOL

    IMEWEKWA AGOSTI 14, 2013 SAA 4:39 USIKU
    MSHAMBULIAJI aliye katika wakati mgumu, Luis Suarez amekanusha taarirfa kwamba leo alisema yuko tayari kurudi kazini na kubaki Liverpool.
    Mchezaji huyo anayetakiwa na Arsenal amenukuliwa katika mahojiano kutoka nchini Japan na gazeti la Uruguay, El Observador akisema angebaki Anfield kwa sababu ya jinsi aanvyoungwa mkono na mashabiki wa Liverpool.
    Lakini akizungumza baada ya kuiwezesha Uruguay kuifunga Japan 4-2 katika mchezo wa kirafiki, Suarez alikanusha na kusema hajabadilisha moyo wake.
    "Sikusema hivyo, labda mtu mwingine alifanya hivyo na kitu cha msingi ni kwamba, nipo hapa kwa sasa na timu ya taifa," Shirika la Habari la Japan, Kyodo limenukuu akisema.
    Luis Suarez
    Luis Suarez
    Furaha: Luis Suarez, akishangilia kuifungia Uruguay, alikakaririwa akisema ameamyua kubaki Liverpool
    In action: Suarez turned out for Uruguay on Wednesday against Japan in a 4-2 win
    Kazini: Suarez alikuwepo kwenye kikosi cha Uruguay leo kilichoifunga Japan 4-2
    In full flight: Suarez claimed the fans' loyalty has won him over despite earlier demanding to leave
    Katika mpambano kamili: Suarez alidaiwa kusema upendo wa mashabiki unamfanya abaki, kabla ya kukanusha taarifa hizo
    Dynamic duo: Suarez (left) celebrates with striking partner Diego Forlan after scoring Uruguay's third goal
    Wakali wawili: Suarez (kushoto) akishangilia na mshambuliaji pacha wake, Diego Forlan baada ya kuifungia bao la tatu Uruguay

    Arsenal imekwishatoa ofa mbili kwa ajili ya mshambuliaji huyo na zpote zimepigwa chini na sasa inajipanga kwa ofa ya tatu ya Pauni Milioni 50.

    TAARIFA ZA UTATA KUHUSU SUAREZ MAJIRA HAYA YA JOTO

    Juni 17 Suarez asema anataka kuondoka Liverpool wakati akiwa na timu yake ya taifa, Uruguay
    Julai 8 Suarez asema anavutiwa na nia ya Arsenal kumsajili
    Julai 17 Wakala wa Suarez aziambia klabu kutoa ofa ya Pauni Milioni 40 kuvunja Mkataba wake
    Julai 24 Arsenal yatoa ofa ya Pauni Milioni 40 jumlisha Pauni 1 kwa ajili ya Suarez 
    Julai 24 Mmiliki wa Liverpool, John W Henry alitweet; "Unafikiria nini juu ya wanachofanya kule Emirates?'
    Julai 30 Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers asema Liverpool haijapokea ofa yoyote juu ya Suarez inayolingana na thamani yake.
    Agosti 4 Suarez aibuka katika mechi ya kumuaga Steven Gerrard
    Agosti 6 Suarez aachwa kikosi cha Liverpool kilichokwenda kucheza mechi ya kirafiki Norway kwa sababu ya majeruhi
    Agosti 7 Suarez awawakia Liverpool kwa kukiuka makubaliano yao ya kumruhusu kuondoka
    Agosti 10 Rodgers asistiza Suarez hauzwi
    Agosti 11 Rodgers asema Suarez lazima aombe radhi kwa kauli yake ili arejeshwe kwenye timu
    Agosti 12 Suarez agoma kuomba radhi, bado anaamini klabu imemsaliti.
    Agosti 12 Rodgers asema uhusiano kati ya Suarez na klabu unaweza kurekebishwa.
    Agosti 14 Chombo cha Habari Uruguay chamnukuu Suarez akisema anataka kubaki Anfield
    Agosti 14 Suarez akanusha kusema anataka kubaki baada ya ushindi wa Uruguay dhidi ya Japan
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NGOMA INOGILE SAKATA LA SUAREZ, SASA AKANA KUSEMA ANATAKA KUBAKI LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top