Na Prince Akbar na Boniface Wambura, IMEWEKWA AGOSTI 14, 2013 SAA 8: 22 MCHANA
HATIMA ya mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara akiwa na jezi ya Yanga SC ya Dar es Salaam msimu huu, inatarajiwa kujulikana keshokutwa, Ijumaa.
Hiyo inafuatia kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kupitia usajili wa wachezaji kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza keshokutwa (Agosti 16 mwaka huu) saa 4 asubuhi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, iliyokuwa ikutane jana (Agosti 13 mwaka huu) na leo (Agosti 14 mwaka huu), Alex Mgongolwa amepanga tarehe hiyo mpya baada ya kikao cha jana kushindwa kupata akidi.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ina wajumbe saba, na ili kikao kiweze kufanyika ni lazima wapatikane wajumbe kuanzia wanne.
Suala ambalo linasubiriwa kwa hamu na wengi kutoka kwenye kikao hicho ni hatima ya Ngassa aliyesaini Yanga SC akitokea Simba SC.
Ngassa alisaini Yanga baada ya kuitumikia Simba SC kwa mwaka mmoja akitokea Azam FC, akiwaambia viongozi wa Jangwani amemaliza Mkataba wake Msimbazi.
Lakini baadaye Simba SC ikaibua Mkataba iliyosaini na Ngassa na inaonyesha anatakiwa kufanya kazi Msimbazi kwa mwaka mmoja mwingine.
TFF nayo ikathibitisha, inao Mkataba ambao Ngassa alisani na Simba SC- lakini kwa kuwa mchezaji mwenyewe amekana kuwa na Mkataba, suala lake sasa litaamuliwa na Kamati ya Mgongolwa Ijumaa.
Lakini kikao cha kujadili hatima ya Ngassa kinakuja siku moja kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii, ambao Yanga itacheza na Azam FC Jumamosi. Maana yake, mchezaji huyo anaweza kujua kama atacheza au hatacheza saa chache kabla ya mechi.
Na huu ni mtihani zaidi kwa kocha wa Yanga, Mholanzi, Ernie Brandts ambaye ameonekana kumuhusisha Ngassa katika programu yake ya mchezo wa Jumamosi.

![]() |
| Atacheza Jangwani? Ngassa akisaini Yanga miezi iliyopita |
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ina wajumbe saba, na ili kikao kiweze kufanyika ni lazima wapatikane wajumbe kuanzia wanne.
Suala ambalo linasubiriwa kwa hamu na wengi kutoka kwenye kikao hicho ni hatima ya Ngassa aliyesaini Yanga SC akitokea Simba SC.
Ngassa alisaini Yanga baada ya kuitumikia Simba SC kwa mwaka mmoja akitokea Azam FC, akiwaambia viongozi wa Jangwani amemaliza Mkataba wake Msimbazi.
Lakini baadaye Simba SC ikaibua Mkataba iliyosaini na Ngassa na inaonyesha anatakiwa kufanya kazi Msimbazi kwa mwaka mmoja mwingine.
![]() |
| Au atabaki Simba SC; Ngassa akikabidhiwa jezi ya Simba SC na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu' mwaka jana |

.png)