• HABARI MPYA

    Wednesday, August 14, 2013

    UCHAGUZI TFF KUFANYIKA OKTOBA 18

    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA AGOSTI 14, 2013 SAA 8:10 MCHANA
    UCHAGUZI wa Kamati ya mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utafanyika Oktoba 20 mwaka huu, imeelezwa. 
    Taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF leo mchana, imesema kwamba, uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPL Board) utatangulia Oktoba 18 mwaka huu.
    Akitangaza mchakato huo wa uchaguzi leo (Agosti 14 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni amesema nafasi zitakazogombewa kwa upande wa TFF ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.
    Nishauri, nichukue fomu? Jamal Malinzi kushoto anatarajiwa kugombea Urais.  

    Fomu kwa wagombea zitatolewa kuanzia Agosti 16 mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 kamili jioni kwenye ofizi za TFF. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti 20 mwaka huu. Fomu kwa nafasi ya Rais ni sh. 500,000, Makamu wa Rais ni sh. 300,000 wakati wajumbe ni sh. 200,000.
    Mbwezeleni amesema kwa wale ambao walilipia fomu katika mchakato uliofutwa na wanakusudia kugombea nafasi zilezile walizolipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.
    Bado unataka Urais? Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi, kaka wa Jamal Malinzi akiwa na Athumani Nyamlani, anayetarajiwa kugombea Urais pia. Kulia ni Ramadhani Nassib anayetarajiwa kugombea Umakamu wa Kwanza. 

    Kwa upande wa uchaguzi wa TPL Board, fomu zitaanza kutolewa Agosti 16 hadi 20 mwaka huu, na nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambapo ada ni sh. 200,000 wakati wajumbe wa Bodi ada ni sh. 100,000.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: UCHAGUZI TFF KUFANYIKA OKTOBA 18 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top