• HABARI MPYA

    Monday, August 12, 2013

    NGASSA AENDELEA KUSOTEA JEZI YANGA SC, SASA AHAMIA 17

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA AGOSTI 12, 2013 SAA 1:18 ASUBUHI
    MRISHO Khalfan Ngassa ameendelea kusotea jezi ya kuvaa katika klabu yake mpya, Yanga SC baada ya jana kuhamia katika jezi namba 17, badala ya tisa aliyovaa katika mechi dhidi ya 3Pillars ya Nigeria.
    Akiichezea Yanga katika mechi ya kwanza tangu arejee baada ya kuondoka mwaka 2010 kwenda, Azam FC, Ngassa alivaa jezi namba tisa (9) wiki iliyopita, badala ya nane (8) alityokuwa akivaa kabla ya kuhama.
    Namba 17; Ngassa jana alivaa jezi namba 17 badala ya tisa

    Na jana katika mechi na SC Villa ya Uganda, Ngassa aliingia uwanjani na jezi namba 17 na akafanikiwa kufungua akaunti mpya ya mabao Jangwani, akiifungia timu hiyo bao moja katika ushindi wa 4-1.
    Ngassa amerejea Yanga SC wakati ambao jezi namba nane anavaa Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima ambaye amegoma kuiachia.
    Akiwa Azam FC alikuwa anavaa jezi namba 16 na aliendelea kuvaa jezi hiyo hata alipohamia Simba SC ambako mwishoni mwa msimu alihamia katika namba nane, lakini aliporejea Yanga SC amekuta namba 16 anavaa Nizar Khalfan, ambaye naye amegoma kuiachia.
    Katika mechi na 3Pillars, Ngassa alichukua jezi namba tisa, ambayo msimu uliopita ilikuwa inavaliwa na Omega Seme aliyetolewa kwa mkopo Prisons ya Mbeya msimu huu. Jezi namba 17 aliyovaa jana ilikuwa haina mtu. 
    Tayari mshambuliaji mpya, Hussein Javu aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar, amechukua jezi namba 21, ambayo iliachwa na Didier Kavumbangu tangu mwanzoni mwa mzunguko wa pili katika Ligi Kuu msimu uliopita.
    Pamoja na hayo, Ngassa yupo hatarini kutocheza Ligi Kuu msimu ujao, kutokana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuthibitisha bado ana Mkataba na Simba SC.
    Juzi Simba SC ikicheza na SC Villa katika mchezo uliokwenda sambamba na sherehe za Simba Day, ilimtambulisha Ngassa kama sehemu ya wachezaji wa kikosi chake msimu huu.
    Yanga SC baada ya kuingia Mkataba na Ngassa, haijajisumbua kumalizana na klabu yake, Simba SC maana yake hataruhusiwa kucheza msimu ujao- vinginevyo ithibitike kama anavyodai mwenyewe hana Mkataba na Msimbazi.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NGASSA AENDELEA KUSOTEA JEZI YANGA SC, SASA AHAMIA 17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top