• HABARI MPYA

    Monday, August 12, 2013

    ARSENAL WANAVYOMTIA 'QIBLI' SUAREZ, AGOMA KUOMBA RADHI LIVERPOOL NA YUKO TAYARI KUFANYA MAZOEZI PEKE YAKE MILELE

    IMEWEKWA AGOSTI 12, 2013 SAA 1:28 ASUBUHI
    UHUSIANO wa Luis Suarez na Liverpool utaingia katika hatua nyingine wiki hii, baada ya mshambuliaji huyo kukataa kuiomba radhi klabu kwa kauli zake kwamba alikubaliana na kocha ataondoka, kulazimisha kutimkia Arsenal.
    Vyanzo vya karibu na mwanasoka huyo wa Uruguay vinaamini uhusiano wake na kocha Brendan Rodgers umeharibika kutokana na kutaka kuondoka Merseysiders kipindi hiki. 
    Suarez anafanya mazoezi peke yake kwenye viwanja vya mazoezi vya Liverpool, Melwood, na Rodgers amesema hatamruhusu kujiunga na timu yake hadi aombe radhi kwa kauli yake ya wiki iliyopita, akiweka wazi anataka kuhamia Emirates.
    Luis Suarez
    Kivyake: Suarez amelazimishwa kufanya mazoezi peke yake na ataendelea kufanya hivyo hadi aombe radhi
    Luis Suarez
    Brendan Rodgers
    Hasira: Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema Luis Suarez hataruhusiwa kujiunga na kikosi chake hadi aombe radhi

    Lakini BIN ZUBEIRY kupitia Sportsmail inafahamu kwamba Suarez hataomba radhi, akiamini amesalitiwa na kocha Rodgers juu ya makubaliano waliyofikia. 
    Anaamini wamekiuka makubaliano ya kiungwan waliyofikia kwamba, Liverpool, isipofuzu Ligi ya Mabingwa ataruhusiwa kuondoka.
    Arsenal tayari imetoa ofa ya Pauni 40,000,001 kwa ajili ya kumnunua mchezaji huyo, lakini imepigwa chini.
    Arsene Wenger
    Anasotea kifaa: Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger tayari ofa zake mbili za kumnunua Luis Suarez zimepigwa chini Liverpool
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENAL WANAVYOMTIA 'QIBLI' SUAREZ, AGOMA KUOMBA RADHI LIVERPOOL NA YUKO TAYARI KUFANYA MAZOEZI PEKE YAKE MILELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top