Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya


CHELSEA WAZITOLEA NJE PAUNI MILIONI 30 ZA MAN CITY KUMTAKA DAVID LUIZ

Chelsea imekataa ofa ya pauni Milioni 30 kutoka Manchester City kutaka kumnunua beki wao, wa Kibrazil, David Luiz mwenye umri wa miaka 30. City inakabiliwa na tatizo la beki, na Micah Richards anatakiwa kuwa nje kwa wiki 10 kwa sababu ya majeruhi.
Borussia Dortmund imethibitisha ofa kibao kwa ajili ya mshambuliajo wao, Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 24, ikizungumzia tetesi za mchezaji huyo kutakiwa na  Manchester United na Chelsea.
Robert Lewandowski
Robert Lewandowski anatakiwa na Chelsea na Manchester United
Mmiliki wa Liverpool, John W Henry yuko tayari kuuzwa kwa viungo Charlie Adam na Jay Spearing -ili kutafuta fedha za kumnunua nyota wa Fulham, Mmarekani Clint Dempsey.
Klabu mbili za Milan, Inter na AC, zinagombea saini ya thamani ya pauni Milioni 8 ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi,Nigel de Jong, mwenye umri wa miaka 27, kutoka Manchester City. De Jong, ambaye alijiunga na City akitokea Hamburg kwa pauni Milioni 18, Januari 2009, amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake Manchester na anaweza kuondoka.
Newcastle inamtaka mshambuliaji wake wa zamani, Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23, kwa mkopo acheze msimu mzima kutoka Liverpool huku ikiwa na pendekezo la kumnunua moja kwa pauni Milioni 12, lakini kocha wa Wekundu hao, Brendan Rodgers hayuko tayari kukubali ofa ya aina hiyo.
Ombi la Michael Dawson kuhamia QPR kutoka Tottenham limeingia zengwe, na Sunderland na Stoke sasa zinatumai kumsajli beki huyo mzoefu wa England mwenye umri wa miaka 28 kwa pauni Milioni 10.
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Eduardo, mwenye umri wa miaka 29, amesema hakuwahi kujua kama alikuwa anatakiwa na Fulham kwa pauni Milioni 7, lakini amesema ni bora aondoke klabu yake ya sasa, Shakhtar Donetsk na kujiunga na klabu yoyote ya Ligi Kuu ya England.
West Ham na Sunderland zinagombea saini ya mchezaji wa West Brom, Peter Odemwingie.
Tottenham imeambiwa ipandishe ofa yake kwa kipa wa Lyon, Hugo Lloris, mwenye umri wa miaka 25, baada ya ofa yao ya awali kwa kipa huyo wa kimataifa wa Ufaransa, kukataliwa na klabu hiyo ya Ligue 1.
Jesus Navas
Jesus Navas anaweza kutua Arsenal
Spurs tayari imeongeza ofa yake kwa mchezaji mwingine - Andre Villas-Boas anamtaka mshambuliaji mwenye umri wa miaka 23, Leandro Damiao acheze pamoja na Emmanuel Adebayor.
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema yuko tayari kumtoa kwa mkopo kiungo wa kimataifa wa Uturuki, Nuri Sahin katika klabu ya England, lakini hawezi kujali kama atakwenda Arsenal, Liverpool au Tottenham. 
Mourinho pia amekanusha kwamba Kaka atapelekwa kwa mkopo Manchester United, kwa sababu ya kusajiliwa kwa winga wa Tottenham, Luka Modric.
Theo Walcott akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake,  Arsenal inajipanga kwa lolote kwa kutaka kumsajili nyota wa Sevilla, Jesus Navas. Mchezaji wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 26 anaweza kuuzwa kwa pauni Milioni 35, lakini klabu yake inaweza kupokea fedha chini ya kiwango hicho.

WALIOONDOKA ARSENAL WANEEMEKA, WALIOBAKI NI 'FULL MAJALALA' 

Wachezaji ambao wameondoka Arsenal kwa miaka saba iliyopita, wameshinda Medali 44 baina yao na klabu 11 tofauti, wakati waliobaki Emirates bado watupu.