• HABARI MPYA

    Thursday, August 30, 2012

    REAL WATWAA SUPER CUP HISPANIA

     Real wakiwa na Super Cup Cup yao
    Ronaldo
    Higuain

    MADRID, Hispania
    KLABU ya Real Madrid imetwaa taji lake la kwanza la Super Cup ya Hispania ndani ya miaka minne kufuatia mabao ya Gonzalo Higuain na Cristiano Ronaldo kuwapa ushindi wa 2-1 dhidi ya Barcelona waliomaliza mechi wakiwa 10 usiku wa kuamkia leo.
    Ushindi huo dhidi ya Barca, iliyompoteza Adriano aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 28 tu ya mchezo huo, ulifanya matokeo ya jumla ya mechi mbili za kuwania taji hilo, yawe 4-4, baada ya Wakatalunya hao kushinda 3-2 katika mechi ya kwanza Uwanja wa Nou Camp na Real wakapewa taji kwa sheria ya mabao ya ugenini.
    Kocha Mreno, Jose Mourinho aliinuka kushangilia mabao yote ndani ya dakika 20 tu za mwanzo, la kwanza dakika ya 11 kwenye Uwanja wa Bernabeu, mfungaji Higuain akitumia mwanya wa makosa ya safu ya ulinzi ya Barca na dakika na dakika nane baadaye Ronaldo akafunga la ushindi.
    Lionel Messi aliifungia Barca bao la kufutia machozi kabla ya mapumziko kwa mpira wa adhabu, akifumua shuti kutoka umbali wa mita 30.
    Pedro aliokolewa mchomo mmoja mkali sana na Iker Casillas dakika 30 kuelekea mwisho wa mechi hiyo na timu zote zilipata nafasi za kuongeza mabao, lakini bahati ilikuwa upande wa Real jana kumaliza ubabe wa miaka mitatu mfululizo wa Barca katika taji hilo.
    Mechi hiyo ilifufua matumaini na furaha ya kikosi cha Mourinho, ambacho kilipoteza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Hispania, La Liga kwa kufungwa 2-1 na Getafe Jumapili.
    (Imeandikwa na Iain Rogers, imetafsiriwa na Mahmoud Zubeiry)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REAL WATWAA SUPER CUP HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top