Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya


ARSENAL KUMSAJILI ESSIEN, MAN UNITED YASUKA KIKOSI CHA LIGI YA MABINGWA

Arsenal inataka kufanya usajili wa ghafla na wa kushitua wa kiungo wa Chelsea, Michael Essien. Arsene Wenger anamtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 kwa mkopo baada ya mambo yake kumuendea kombo Stamford Bridge.
Washika Bunduki hao wa Londin, pia wako tayari  kumtoa kwa mkopo Marouane Chamakh, mwenye umri wa miaka 28, kwenda Malaga au Besiktas.
Michael Dawson
Michael Dawson anaweza kuondoka tu White Hart Lane
Chelsea inajiandaa kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Daniel Sturridge, mwenye umri wa miaka 22, kama watafanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji wa Bayer Leverkusen, Andre Schurrle. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anaweza kugharimu pauni Milioni 20.
Beki wa Tottenham na England, Michael Dawson, mwenye umri wa miaka 28, anaweza kuondoka tu White Hart Lane, licha ya kwamba majeruhi ya Younes Kaboul yanaweza kumuweka nje ya uwanja hadi Krisimasi.
Everton inataka kumsajili kiungo wa Blackburn, Steven N'Zonzi baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kutofautiana na kocha wa Rovers, Steve Kean.
Huddersfield inatumai kuwasajili mshambuliaji wa QPR , DJ Campbell, mwenye umri wa miaka 30, na mchezaji wa Leicester, Jermaine Beckford, mwenye umri wa miaka 28, kuziba pengo la mchezaji wa kimataifa wa Scotland, Jordan Rhodes, mwenye umri wa miaka 22, ambaye amejiunga na Blackburn jana.
Nicklas Bendtner
Bendtner anatakiwa na Stoke na Juventus
Mshambuliaji wa Arsenal, Nicklas Bendtner, mwenye umri wa miaka 24, amepewa ofa na Stoke City ya kusajiliwa kwa mkopo, lakini klabu nyingine kadhaa zinawasiliana na mwakilishi wake.
Au mshambuliajki huyo wa Arsenal anaweza kwenda Juventus baada ya kukubali ofa ya kujiunga na mabingwa hao wa Serie A.

FLETCTHER KUCHEZA ULAYA

Kiungo wa Manchester United, Darren Fletcher anatarajiwa kutajwa kwenye kikosi cha Ligi ya Mabingwa cha United, licha ya kwamba hajacheza mechi yoyote ya ushindani tangu Novemba.
Dimitar Berbatov, mwenye umri wa miaka 31, sasa anafanya kila liwezekanalo kuhakikisha anakamilisha uhamisho wake kwenda Fulham kutoka Manchester United.

CELTIC SI WAMFANYIA 'USHENZI' BANGURA 

Nyota wa Celtic, Mohamed Bangura alifanyiwa mambo yasiyo ya kiungwana kabla ya kuondoka kwa mkopo kwenda AIK.