• HABARI MPYA

    Tuesday, August 28, 2012

    MANUNDU SHOOTING YAPANIA KUFIKA MBALI

    Suleiman Mvungi (mwenye mpira) wa Manundu FC akitafuta mbinu za kuchomoka katika mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na Ligi Daraja la Nne Korogwe jana, Uwanja wa Manundu Sokoni. Kushoto kwake ni Jackson Raphael na kulia ni Jackson Chale wakati katikati ni Michael Sempoli.


    Na Prince Akbar
     Kocha Ahmad Kabwere
    KOCHA wa klabu ya Manundu Shooting ya Korogwe, Tanga- Ahmad Kabwere amesema kwamba wameanza maandalizi ya Ligi Daraja la Nne ngazi ya wilaya, wakiwa na dhamira ya kufika mbali msimu huu.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwenye Uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, Manundu Sokoni, Kabwere alisema wapo kwenye hatua ya awali ya maandalizi baada ya kukamilisha usajili wa kikosi kipya kabisa, kufuatia kufukuzwa kwa wachezaji wote wa zamani kwa utovu wa nidhamu.
    “Wachezaji hawa unaowaona hapa, wote ni wapya, baada ya wale wa awali wote kufukuzwa kwa utovu wa nidhamu na tunashukuru wanaonyesha uwezo mkubwa na kutia matumaini, naamini kabisa tutafika mbali kwenye ligi,”alisema.
    Kabwere ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Korogwe kuanzia 2001 hadi 2007, alisema kwamba wachezaji wapya wameonyesha nidhamu ya hali ya juu na uwezo pia.
    “Wengi wao kama unavyowaona ni vijana wadogo haswa na wengi ni wanafunzi, wana nia ya kujifunza na kufika mbali, ni washindani na hilo wamelidhihirisha hata katika mechi za kirafiki ambazo tumecheza hadi na timu kutoka Dar es Salaam,”alisema kocha huyo mzoefu.
    Mafanikio makubwa ya Manundu Shooting kihistoria ni kuchukua ubingwa wa Wilaya, katika mwaka wake wa kwanza wa kuanzishwa, 1994 na mwaka huu wamepania kuvunja rekodi hiyo kwa kuhakikisha wanafika Ligi ya kanda.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANUNDU SHOOTING YAPANIA KUFIKA MBALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top