• HABARI MPYA

    Thursday, August 30, 2012

    TWITE KUFIKIA MIKONONI MWA POLISI LEO?

    Twite aikabidhiwa jezi ya Yanga na Abdallah Bin Kleb, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga baada ya kukamilisha usajili

    Na Mahmoud Zubeiry
    LINAWEZA kutokea bonge la sinema leo Dar es Salaam na sterling sijui atakuwa nani. Beki Mbuyu Twite imeelezwa anawasili leo Dar es Salaam kujiunga na klabu yake, Yanga SC akitokea Kigali, Rwanda alipokwama kwa shughuli za kifamilia.
    Wakati huo huo, viongozi wa Simba imeelezwa wamekaba njia zote za kuingilia nchini wakiwa na RB ya kumkamata beki huyo wa kimataifa wa Rwanda, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa tuhuma za kuwatapeli dola za Kimarekani 30,000.
    Inadaiwa, kabla ya kusaini Yanga, Twite aliyekuwa akichezea APR ya Rwanda alisaini Simba na kuchukua dola 30,000.
    Hata hivyo, baadaye mchezaji huyo alighairi na kuamua kwenda Yanga na kurudisha fedha za Simba kupitia viongozi wa APR na St Eloi Lupopo ya DRC, ambazo zilikuwa zinammiliki kwa pamoja mchezaji huyo.
    Lakini viongozi wa Simba waligoma kupokea fedha hizo ingawa viongozi wa APR na Lupopo walifika hadi ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka kuzikabidhi fedha hizo, ili Simba wakazichukulie hapo.
    Twite aliianza kuichezea Yanga wiki iliyopita ilipokuwa Kigali, Rwanda kwa ziara ya wiki moja lakini alishindwa kurejea na wenzake Jumatatu kwa kile kilichoelezwa anakamilisha kuhama kwake rasmi na kuja kuanza maisha mapya Dar es Salaam,
    Lakini upande wa pili, Simba SC waliamini beki huyo amekwepa kukamatwa kufuatia kuvuja kwa habari za mpango wa kumtegea akitua nchini wamkamate. Je, beki huyo atatua leo, na kama atatua Simba watamkataba kweli, na kama watamkamata, Yanga watakubali?
    Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona picha hilo litakuwaje kama litatokea.     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWITE KUFIKIA MIKONONI MWA POLISI LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top