• HABARI MPYA

    Tuesday, August 28, 2012

    COASTAL UNION WAWEKWA KITI MOTO

    Kocha Mgunda akizungumza na wachezaji

    Kocha Mgunda akizungumza na wachezaji

    Kocha Mgunda akizungumza na wachezaji

    Kocha Mgunda kulia, na Msaidizi wake Kondo

    Wachezaji wakimsikiliza kocha wao

    Viongozi; kutoka kulia, Mwenyekiti Ally Ahmad Hilal ‘Aurora’, Katibu Kassim El Siagi na Meneja Akida

    Kulia ni Nahodha Said Swedi ‘Panucci’ akiwa na wachezaji wenzake wakimskiliza kocha

    Mafaza; Kulia ni Razack Khalfan, nyuma yake Jackson Chove, nyuma kabisa Juma Mpongo na mbele yake kushoto ni Suleiman Kassim ‘Selembe’

    Wa kwanza kulia Aziz Gilla, anayemfuati ni Jerry Santo na mbele yao ni Juma Jabu, ambao wote walikuwa Simba SC

    Kushoto ni Pius Kisambale

    Na Mahmoud Zubeiry, Tanga
    BAADA ya jana kuonyesha kiwango duni, wakimenyana na JKT Oljoro ya Arusha pamoja na kushnda bao 1-0, Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, wachezaji wa Coastal Union leo asubuhi wamewekwa ‘kiti moto’ na makocha wao baada ya mazoezi ya asubuhi, kwenye Uwanja huo.
    Kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda aliwaleza wazi wachezaji wa timu hiyo matatizo yao ya kiuchezaji akitolea mfano mechi mbili zilizopita, ya jana dhidi ya Oljoro na Polisi mjini Morogoro.
    Alitumia takriban saa nzima akizungumza na wachezaji hao, ambao walionekana kutulia wakimsikiliza kwa makini.
    Katika mchezo wa jana wa kirafiki, kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanza Septemba 15, bao pekee la mabingwa hao wa 1988, lilitiwa kimiani na beki mpya aliyesajiliwa kutoka Simba SC, Juma Jabu dakika ya 32 baada ya kupanda mbele kusaidia mashambulizi akiteleza kutokea wingi ya kushoto.
    Huo ni ushindi wa kwanza wa Wagosi hao wa Kaya, ndani ya mechi tatu zsa kujipima nguvu, ikitoka kufungwa 3-2 na Bandari mjini Mombasa, Kenya na 1-0 dhidi ya Polisi mjini Morogoro.
    Pamoja na ushindi huo, mashabiki wa Coastal hawakuridhishwa na kiwango cha timu na kuanza kubeza uwezo wa makocha wa timu hiyo, Juma Mgunda na msaidizi wake, Habib Kondo.
    Habari za ndani zinasema kwamba Coastal inafikiria kubadilisha benchi la ufundi kutokana na kutoridhishwa na uwezo wa timu.   
    Coastal iliwekeza kwenye usajili wa kishindo, ikiamini itafanya vizuri katika Ligi Kuu, lakini kwa matokeo haya ya awali tayari hofu imeanza kuingia na wakati mashabiki wakitilia hofu uwezo wa makocha, wengine wanatilia hofu uwezo wa wachezaji waliosajiliwa, wakiamini inaweza kuwa ni bora kwa majina tu.
    Kikosi cha Coastal kinaundwa na makipa; Juma Mpongo, Abraham Chove na Rajab Kaumba, mabeki; Said Sued (Nahodha) Mbwana Kibacha (Nahodha Msaidizi) Othman Omary, Juma Jabu, Ismail Suma, Jamal Machelenga, Cyprian Lukindo na Philipp Mugenzi.
    Viungo watakuwa ni Jerry Santo, Razack Khalfan, Mohamed Binslum, Khamis Shango, Mohamed Issa, Mohamed Soud, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Lameck Dayton, Joseph Mahundi, Aziz Gilla na Shaffih Kaluani, wakati washambuliaji ni Nsa Job, Atupele Green, Danny Lianga na Pius Kisambale.
    Mbali na Kocha Mkuu, mshambuliaji wake wa zamani, Mgunda,  na Msaidizi wake, beki wa zamani wa Pan African, Habibu Kondo, benchi la ufundi la Coastal linakamilishwa na kocha wa viungo, mchezaji wake wa zamani, Ally Jangalu na kocha wa makipa Bakari Shime.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION WAWEKWA KITI MOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top