• HABARI MPYA

    Sunday, August 26, 2012

    SIMBA SC NA TIMU YA OLIECH LEO ARUSHA

    Simba SC

    Na Mahmoud Zubeiry
    KATIKA kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii, mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC, leo watacheza mechi ya kujipima nguvu na Mathare United ya Kenya kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
    Mathare inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, ambayo ilimuibua kisoka mshambuliaji wa AJ Auxerre ya Ufaransa, Dennis Oliech inatarajiwa kuwasili leo asubuhi Arusha tayari kwa mchezo huo.
    Simba itamenyana na Azam katika mechi ya Ngao ya Jamii ya kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Septemba 8, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kuchelewa kwa mechi hiyo ambako kumeenda sambamba na kuchelewa kuanza kwa ligi hiyo, kumetokana na kuchelewa kufikiwa mwafaka mapema wa mkataba mpya wa udhamini wa Ligi Kuu.
    Mkataba wa awali wa Vodacom na TFF unafikia tamati mwishoni mwa mwezi huu na kusainiwa mkataba mwingine, baada ya majadiliano yanayoendelea.
    Lakini kwa kuwa Mkutano Mkuu wa TFF uliopita uliridhia kuanzia msimu ujao Ligi Kuu iendeshwe na kampuni itakayoundwa na klabu za Ligi Kuu mjadala kuhusu udhamini mpya wa ligi umekuwa mrefu kutokana na kuhusisha pande tatu, klabu, wadhamini na shirikisho.
    Lakini sasa, kwa vyovyote, hata maridhiano ya mkataba mpya wa udhamini na Vodacom yachelewe tena, mechi hiyo itachezwa Septemba 8, ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.
    Kihistoria hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili kuishirikisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
    Mtibwa ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao 2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
    Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga Yanga mabao 2-0. 

    MABINGWA WA MECHI ZA NGAO YA JAMII:
    Mwaka          Mshindi        Matokeo 
    2001             Yanga           2-1 Simba
    2010             Yanga           0-0 Simba (3-1penalti)
    2011             Simba           2-0 Yanga
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC NA TIMU YA OLIECH LEO ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top