• HABARI MPYA

    Wednesday, August 29, 2012

    MBONGO KUKIPIGA UJERUMANI, TFF YATAKIWA KUTUMA ITC HARAKA AANZE KAZI


    CHAMA cha Soka Ujerumani (DFB) kimetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Robert Makanja ili aweze kucheza mpira wa miguu nchini humo.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, DFB imetuma maombi hayo TFF ili kumwezesha mchezaji huyo kuichezea timu ya TUS Ahausen, Hessischer FuBall-Verband ambayo hata hivyo haikuelezwa iko ligi ya daraja gani nchini humo.
    Kwa mujibu wa Mkuu wa Mashindano wa DFB, Markus Stenger, Mtanzania huyo ameombewa hati hiyo kama mchezaji wa ridhaa kwa maelezo kuwa hakuwahi kusajiliwa na klabu yoyote nchini.
    TFF inafanyia kazi maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya taratibu husika kukamilika ikiwemo kubaini kama kweli mchezaji huyo hakuwahi kusajili na klabu yoyote hapa nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBONGO KUKIPIGA UJERUMANI, TFF YATAKIWA KUTUMA ITC HARAKA AANZE KAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top