• HABARI MPYA

    Tuesday, August 28, 2012

    TUSKER KUDHAMINI KOMBE LA CHALLENGE, YATOA MPUNGA LEO KAMPALA

    Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye akizungumza na mwasisi wa CECAFA, Kezekia Ssegwanga Musisi kabla ya uzinduzi wa michuano ya mwaka huu ya Tusker katika hoteli ya Serena mjini Kampala leo.

    Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye akipokea Kombe la mwaka huu la Tusker kutoka kwa Mutahi katika hoteli ya Serena mjini Kampala leo. Kulia ni rais wa FUFA, Livingstone Kyambadde.

    Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Afrika Mashariki (EABL), Lemmy Mutahi  (katikati) akikabidhi mfano wa hundi kwa Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye. Kulia kabisa ni rais wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Livingstone Kyambadde mjini Kampala leo.


    Na Mahmoud Zubeiry
    KAMPUNI ya Bia Afrika Mashariki (EABL), kupitia bia yake ya Tusker Lager, leo imetangaza udhamini wa dola za Kimarekani 450,000 kwa ajili ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la CECAFA –Tusker Challenge Cup itakayofanyika mjini Kampala, Uganda.
    Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) pia imesema mashindano hayo yataanza Novemba 24 kwenye Uwanja wa Taifa wa Mandela, Namboole na kufikia tamati Desemba 8.
    Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye alitua Kampala Jumatatu kwa maandalizi ya michuano hiyo na leo wamezindua rasmi kwenye hoteli ya Serena Hotel mjini Kampala na Meneja Masoko wa EABL, Lemmy Mutahi amesema lengo la michuano hiyo ni kuzisaidia maandalizi timu za Afrika Mashariki na Kati katika kuwania tiekti ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
    Musonye alisema udhamini huo ni ongezeko la aslimia 5, kutoka michuano ya mwaka jana mjini Dar es Salaam, ambayo Uganda waliibuka mabingwa.
    Musonye alisema udhamini huo utahusu usafiri, malazi na huduma nyingine, wakati jumla ya dola za Kimarekani 60.000 zitakuwa kwa ajili ya zawadi, bingwa akipewa dola 30.000, tmshindi wa pili dola 20.000 na dola 10.000 mshindi wa tatu.  Musonye alisema mechi zote zitaonyeshwa na Televisheni ya Super Sport.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TUSKER KUDHAMINI KOMBE LA CHALLENGE, YATOA MPUNGA LEO KAMPALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top