• HABARI MPYA

    Wednesday, August 29, 2012

    COASTAL YAPIGWA 2-0 MKWAKWANI NA BANDARI, MGUNDA, KONDO WAKALIA KUTI KAVU

    VICHWA VINAUMA; Makocha wa Coastal, Juma Mgunda kulia na Msaidizi wake, Habib Kondo kushoto

    Na Princess Asia
    COASTAL Union imefungwa mabao 2-0 jioni hii na Bandari ya Mombassa, Kenya katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
    Mabao ya Bandari inayocheza Ligi Daraja la Kwanza Kenya, yalitiwa kimiani na kiungo David Naftali dakika ya 27 kwa shuti la umbali la mita 35, baada ya kupewa pasi na mshambuliaji Thomas Marucie, wote Watanzania.
    Bao la pili lilifungwa na Evan Wandela dakika ya 88 kwa kichwa akiunganisha kona iliyochongwa na Hussein Puzzo.
    Baada ya mchezo huo, mashabiki wa Coastal waliwatia kashikashi makocha Juma Mgunda na Msaidizi wake Habib Kondo wakidai hawafai na kutaka waondolewe, hali ambayo ilifanya waondolewe uwanjani kwa msaada wa Polisi.
    Hali hii inajitokeza kwa mara ya pili, baada ya juzi pia timu hiyo ikicheza na JKT Oljoro ya Arusha pamoja na kushinda bao 1-0, mashabiki walilalamikia kiwango kibovu na kuzomea makocha. Jumamosi, Coastal itacheza Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL YAPIGWA 2-0 MKWAKWANI NA BANDARI, MGUNDA, KONDO WAKALIA KUTI KAVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top