• HABARI MPYA

    Saturday, March 07, 2009

    MATUMLA KUPIGANA PAMBANO LA AMIR KHAN

    Juu: Matumla akipongezwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Frederick Sumaye enzi zake akitamba WBU. Chini Matumla akipigana na Cheka katika pambano lake la mwisho mjini Morogoro mwezi uliopita.

    BONDIA Rashid 'Snake Boy' Matumla, anatarajiwa kuondoka nchini wiki hii kwenda London, Uingereza kuzipiga na bondia Paul Smith, kuwania taji la WBA International, uzito wa Super Middle Jumamosi wiki ijayo.
    Akizungumza na leo mjini Dar es Salaam, Matumla alisema kwamba anajiandaa vizuri kwa ajili ya pambano hilo na anaamini atarejea na mkanda wa ubingwa wa taji hilo nchini.
    "Mimi niko fiti, tena kuliko nilivyokuwa wakati napigana na Cheka, nakwenda nikiwa nina matumaini ya kurejea na mkanda,"alisema Rashid, enzi zake akijulikana kama Snake Boy.
    Matumla, bingwa wa zamani wa dunia WBU, uzito wa Light middle atazipiga na Smith aliyewahi kumtwanga Francis Cheka kwa raundi 12, kwenye ukumbi wa MEN Arena, hilo pambano la utangulizi kabla ya Amir Khan na Barrera. Smith amelazimika kurejea kwenye uzito wa Super-Middle ili kutimiza dhamira yake ya kutwaa taji na amesema amekuwa akijifua vikali kuhakikisha anatwaa taji hilo la dunia.
    Matumla anayekumbukwa kwa rekodi yake ya kupigana mapambano 29 bila kupigwa hadi anatwaa ubingwa wa WBU, atapanda ulingoni kwa mara ya 50 siku hiyo akiwa amepigwa mara kumi na kutoka sare mara moja.
    Smith, ambaye rekodi yake ni kushinda mapambano 25, akiwa amepigwa mara moja amekuwa akijinoa bondia mkali kama Matthew kujiandaa kukabiliana na Matumla ulingoni.
    Matumla japokuwa ana umri wa miaka 40, lakini bado ni miongoni mwa mabondia wakali katika uzito wake duniani.
    Ulaya anakumbukwa zaidi kwa vitu alivyofanya mwaka 1999 alipokwenda kutwaa ubingwa wa dunia wa WBU, kwa kumpiga mtu nyumbani kwao, alimdunda Paolo Pizzamiglio kwa KO raundi ya pili tu mbele ya mashabiki wake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MATUMLA KUPIGANA PAMBANO LA AMIR KHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top