• HABARI MPYA

    Thursday, March 19, 2009

    JENGO LA KISASA YANGA KUZINDULIWA KARIBUNI



    WAKATI sehemu kubwa ya ukarabati wa jengo la makao makuu ya klabu ya Yanga ukielekea kukamilika, mafundi wameanza ujenzi wa chumba cha mazoezi (gym), bwawa la kuogelea pamoja na sehemu ya kuegesha magari ya wachezaji.
    Mwandishi wa habari hizi alitembelea makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani mjini Dar es Salaam jana na kuwakuta mafundi wakiendelea na ujenzi huo ambao utakapo kamilika inakadiriwa utatumia zaidi ya Sh800milioni.
    Mmoja wa mafundi wanaohusika na ujenzi huo aliyejitambusha kwa jina la Misha Msonge ambaye alimtembeza mwandishi wa habari hizi karibu sehemu zote za jengo hilo, alisema kuwa kazi ya ujenzi wa sehemu ya mzoezi ya viungo, na maegesho ya magari ya wachezaji inaweza kuchukua wiki mbili hadi tatu kukamilika kabla ya kuanza kutumika.
    Msonge alisema ukiondoa kazi hiyo mpya waliyoianza sasa, vyumba vilivyotengwa kutumika kwa ajili ya wachezaji vimekalika hivyo kinachosubiriwa na samani zinazotarajiwa kuingizwa muda wakati wowote kuanzia sasa.
    "Nafikiri kama unavyoona ninaweza kusema kazi kubwa imewataanza kulitumia jengo la Yanga ifikapo mwisho wa Machi.kamilika tunachomalizia hapa ni hii sehemu ya bwawa la kuogelea, gym na sehemu ile ambayo ni maegesho ya magari ya wachezaji.
    ìKwenye vile vyumba vya kulala wachezaji tumekwisha kamilisha kinachosubiriwa ni kuingizwa samani ili viweze kutumika," alisema fundi huyo ambaye aliongeza kwa niaba ya mkandarasi ambaye hakutaka kuzungumza na mwandishi.
    Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega alipoulizwa ni lini jengo hilo litaanza kutumika rasmi alisema hawezi kuzungumzia kwa sasa hadi pale watakapokabidhiwa rasmi na mkandarasi.
    Mwezi Januari, Madega aliliambia gazeti hili kuwa wataanza kulitumia jengo la Yanga ifikapo mwisho wa Machi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JENGO LA KISASA YANGA KUZINDULIWA KARIBUNI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top