• HABARI MPYA

    Saturday, March 14, 2009

    YANGA BILA DAKTARI MISRI

    Majuto Omary, Cairo
    MABINGWA wa Tanzania wapo kwenye hatari kubwa ya kuwa na majeruhi wengi baada ya daktari wake, Nassoro Matunzya kushindwa kufuatana na timu kutokana na kuchelewa ndege.
    Matunzya alikuwepo Dar es Salaam wakati msafara wa timu hiyo ulipokuwa unaondoka juzi mchana, lakini alitoweka katika mazingira ambayo hayakufahamika kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere.
    Uongozi wa Yanga ulifanya mpango ili daktari huyo aondoke na ndege ya Ethiopia, hata hivyo haikuweza kueleweka kwa nini hajatokea mpaka sasa.
    Mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega alisema kuwa juhudi zinafanyika ili Matunzya afike kabla ya mchezo uliopangwa kufanyika kesho saa 1:00 za Misri (saa 2 usiku kwa Afrika Mashariki).
    Madega alisema kuwa kama itashindikana, basi wataomba msaada kwa ubalozi wa Tanzania ili kuona kama wataweza kupata msaada wa tabibu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA BILA DAKTARI MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top