• HABARI MPYA

    Saturday, March 28, 2009

    YANGA YAWAPELEKA SHAMBA LA BIBI AL AHLY


    MECHI ya marudiano, raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji Yanga na Al Ahly ya Misri, itachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, zamani Taifa mjini Dar es Salaam, maarufu kama Shamba la Bibi.
    Hiyo inatokana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukubali ombi la Yanga kutaka mchezo dhidi ya mabingwa mara sita Afrika, ufanyike kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
    Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Florian Rweyemamu Kaijage, alisema mchezo huo utafanyika Aprili 4, mwaka huu na kwamba tayari Yanga na TFF zimekubaliana na suala hilo. Hata hivyo, alisema TFF awali haikuwa imekubaliana na Yanga kutokana na ufinyu wa uwanja huo kulinganisha na ukubwa wa mechi hiyo. Lakini alisema Yanga imekubali kuwa itauza kiwango maalumu cha tiketi kwa watazamaji watakaoingia uwanjani. Kaijage alisema TFF ilitaka mchezo huo ufanyike kwenye Uwanja wa Taifa (uwanja mpya), lakini Yanga imesisitiza lazima ufanyike Uwanja wa Uhuru, hivyo wao wakaona hakuna sababu ya kuwakatalia na kuwa Yanga ilikataa ushauri wa kucheza uwanja mpya. Kigezo kikubwa kilichotumiwa na Yanga ni kuwa Uwanja wa Uhuru ndio waliouzoea, hivyo hakuna sababu ya kuhama sehemu nyingine. Kutokana na hali hiyo, mchezo huo sasa utafanyika saa 9 alasiri na kuongeza kuwa siku ya kuwasili nchini kwa Al Ahly haijajulikana. Yanga inanolewa na makocha watatu wa Kiserbia, wakiongozwa na Dusan Kondic (pichani kulia juu), wengine ni Spaso Sokolovoski na Civojnov Serdan.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAWAPELEKA SHAMBA LA BIBI AL AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top