• HABARI MPYA

    Saturday, March 28, 2009

    BUSHOKE KUZINDUA ALBAMU BUKOBA


    MSANII Rutta Bushoke (pichani kulia) anatarajiwa kufanya maonyesho la kutambulisha albamu yake mpya, iitwayo Dunia Njia mjini Bukoba Aprili 12 na 13 mwaka huu.
    Meneja wa mwanamuziki huyo, Athumani Tippo wa Zizzou Fashons, aliiambia bongostaz mjini Dar es Salaam jana kwamba onyesho la kwanza litafanyika kwenye ukumbi wa Lina’s Night Club Aprili 12 wakati la pili litakuwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba .
    Alisema onyesho la Lina’s Night Club, kiingilio kitakuwa Sh. 10,000 kwa kila mtu, wakati Uwanja wa Kaitaba ambalo litaanza alasiri, kiingilio kitakuwa Sh. 1500.
    Tippo alisema katika maonyesho yote hayo, Bushoke, mtoto wa mwanamuziki wa zamani wa bendi ya DDC Mlimani Park ‘Sikinde Ngoma ya Ukaye’, Max Bushoke, atasindikizwa na wasanii wengine nyota wa Bongo Fleva.
    Aliwataja wasanii hao kuwa ni Mwasiti, Maunda Zorro, Man Ngwair, Mr. Blue na Steve E.
    Albamu hiyo iliyotengenezwa na wataalamu mbalimbali, akiwemo Said Comorien, Alan Mapigo, Enrique, inaundwa na vibao vitamu kama Dunia Njia yenyewe, Usiende Mbali, Rain on Me, Lala na nyingine.
    Bushoke alizindua albamu yake ya kwanza iliyoitwa Barua, Okoba 15, mwaka 2004 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam akiwa sambamba na Ngwair aliyezindua albamu yake ya Mikasi, iliyokuwa ina vibao vitamu, Bado Niko, Sikiliza, Dakika Moja, Weekend, Zawadi, Mademu Wangu, She Gotta Gwan, Geto Langu, Napokea Simu na Mikasi wenyewe.
    Barua ilikuwa inaundwa na nyimbo 12, ambazo ni Neema, Christina Bundala, Hunijui, Fukara, Kwani We Ni Nani, Mtu Mzima Ovyo, Nkurukumbi, Kwa Nini, Harusi, Mapenzi Yana Raha, Barua yenyewe na Mume Bwege aliomshirikisha mrembo Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K.Lyinn’.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BUSHOKE KUZINDUA ALBAMU BUKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top