• HABARI MPYA

    Tuesday, July 08, 2014

    PIGO STARS, MKUDE NA HIMID MAO NAO MAJERUHI WAKATI TAYARI TIMU INAMKOSA FRANK DOMAYO

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    VIUNGO wawili wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Jonas Gerard Mkude wa Simba SC na Himid Mao Mkami wa Azam FC ni majeruhi.
    Kocha Mkuu wa Stars, Mholanzi Mart Nooij amesema wachezaji hao wamerejea kutoka Botswana ambako timu hiyo iliweka kambi ya wiki mbili wakiwa majeruhi.
    Maana yake, nyota hao wako shakani kuichezea Stars katika mchezo wa mwisho wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco dhidi ya Msumbiji Julai 20 mwaka huu.
    Himid Mao kushoto ni majeruhi

    Pamoja na hayo, Nooij amesema kambi ya Botswana iliyodumu kwa wiki mbili ilikuwa nzuri na imesaidia kuwajenga wachezaji wake baada ya kufanya mazoezi na kupata mechi tatu za kujipima nguvu.
    Stars ilifungwa mechi mbili, moja dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Botswana mabao 4-2 na nyingine dhidi ya timu ya jeshi la nchini humo, BDF walishinda moja 3-1 na kufungwa moja 2-1.
    Nooij amesema wachezaji hao wapo katika kufanyiwa vipimo mjini Dar es Salaam na baada ya hapo atajua uzito wa matatizo yao na pia kujua hatima yao kuelekea mchezo na Msumbiji.
    Tayari Stars inamkosa kiungo mwingine, Frank Domayo wa Azam FC aliyefanyiwa upasuaji wa nyama za paja nchini Afrika Kusini ambaye anatakiwa kuwa nje ya Uwanja hadi mwakani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO STARS, MKUDE NA HIMID MAO NAO MAJERUHI WAKATI TAYARI TIMU INAMKOSA FRANK DOMAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top