• HABARI MPYA

    Tuesday, July 08, 2014

    MAXIMO AKATISHA SAFARI YAKE KUBADILISHANA NAMBA ZA SIMU NA BOSI WA SIMBA SC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mbrazil Marcio Maximo leo alikatisha safari yake katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Said Tuliy, mbaye mwishowe walibadilishana namba za simu.
    Maximo akiwa na Msaidizi wake, Leonardo Neiva na kiungo mshambuliaji, Andrey Coutinho wote Wabrazil walikuwa wanapita katikati ya Jiji maeneo ya Ohio na Tuliy alikuwa maeneo hayo pia.
    Rafiki wewe Simba kumbe; Maximo kushoto akizungumza na Tuliy kulia leo maeneo ya Ohio

    Maximo baada ya kubadilishana namba za simu na Tuliy
    Maximo anapiga picha na shabiki 

    Wakati Maximo anajiandaa kuvuka barabara, mashabiki wakaanza kumfurahia na kuomba kupiga naye picha.
    Alipomaliza wakati anataka kuondoka, akamuona Said Tuliy anazungumza na mtu, Maximo akarudi na kumuita Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Vijana ya Simba SC na kuanza kuzungumza naye na kubadilishana namba za simu.
    Maximo na Tuliy walikuwa marafiki wakubwa wakati Mbrazil huyo anaifundisha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.
    Hakuna hakika kama Maximo baada ya kukutana tena na Tuliy watarudia urafiki kama wa zamani, kwa sababu kwa sasa wawili hao sasa ni wapinzani wa jadi, mmoja Simba, mwingine Yanga.
    Maximo akizungumza na shabiki
    Maximo anakatiza barabara baada ya kumalizana na Tuliy
    Maximo, Leonard na Coutinho mbele wakivuka barabara
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAXIMO AKATISHA SAFARI YAKE KUBADILISHANA NAMBA ZA SIMU NA BOSI WA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top