• HABARI MPYA

    Thursday, July 17, 2014

    LINA KESSY AUTEULIWA KUWA OFISA MICHEZO AU

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Lina Kessy ameteuliwa kuwa Ofisa Michezo wa Umoja wa Afrika (AU).
    Uteuzi huo umefanywa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Nkozasana Dlamini-Zuma, na Lina atatumikia nafasi hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu katika makao makuu ya AU yaliyopo Addis Ababa, Ethiopia.
    Lina Kessy ameula AY

    Lina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) amewashukuru wote ambao kwa michango yao ya hali na mali imemwezesha kufika hapo.
    Ameishukuru TFF kwa kumlea na kumjenga. Shukrani nyingine amezitoa kwa Serikali kupitia Kurugenzi ya Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).
    TFF inampongeza kwa uteuzi huo, na tunaamini ataipeperusha vyema bendera ya Tanzania ikiwemo kuwa chachu ya maendeleo ya michezo kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LINA KESSY AUTEULIWA KUWA OFISA MICHEZO AU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top