• HABARI MPYA

    Friday, February 14, 2014

    MECHI YA TWIGA STARS, ZAMBIA ‘LIVE’ ZNBC

    Na Boniface Wambura, Lusaka
    KIKOSI cha Twiga Stars kinashuka Uwanja wa Nkoloma, Lusaka nchini Zambia leo kuwavaa wenyeji Zambia (Shepolopolo) katika mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayooneshwa moja kwa moja ‘live’ na televisheni ya Shirika la Taifa la Utangazaji la Zambia (ZNBC).
    Mechi hiyo itaanza saa 9 kamili mchana kwa saa za Zambia ambapo Tanzania itakuwa saa 10 kamili jioni huku Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage akiwa tayari ametangaza ‘silaha’ zake kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza.
    Kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage

    Watakaoanza kupeperusha bendera ya Tanzania katika mechi hiyo ambayo kiingilio ni bure kwa majukwaa yote isipokuwa lile kuu ni; Fatuma Omari 1, Fatuma Bashiru 17, Donisia Daniel 2, Fatuma Issa 5, Evelyn Sekikubo 15, Sophia Mwasikili 16, Vumilia Maarifa 10, Mwapewa Mtumwa 9, Asha Rashid 14, Etoe Mlenzi 13 na Shelida Boniface 7.
    Wachezaji wa akiba ni Maimuna Said 18, Fatuma Hassan 12, Zena Khamis 6, Esther Chabruma 8, Amina Ally 4, Therese Yona 11 na Happiness Hezron 3.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI YA TWIGA STARS, ZAMBIA ‘LIVE’ ZNBC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top