• HABARI MPYA

    Monday, February 24, 2014

    AZAM FC YAOMBA RADHI KWA SOKA 'MBOFUMBOFU' NA MATOKEO MABAYA

    “Uongozi wa Azam FC kwa niaba ya benchi la ufundi na wachezaji, tunaomba radhi kwa mashabiki wetu mnaotupenda na kutuunga mkono kwa matokeo mabovu na mpira mbovu tuliouonesha jana.

    Mpira na matokeo yale havilingani na uwekezaji, huduma na matarajio ya wamiliki, wapenzi na mashabiki wa kweli wa Azam FC, Lengo la uongozi mwaka huu ilikuwa ni kucheza angalau raundi ya makundi ya mashindano ya kombe la shirikisho na pia kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania. Kwa matokeo ya Beira Mozambique na jana Chamazi, ni dhahiri ndoto za mashindano ya kimataifa zimekufa kabisa huku ile ya kutwaa ubingwa wa Tannzania ikiwa rehani.
    Azam FC inawaomba radhi watu wote mlioumizwa na matokeo haya na kama taasisi tutakaa chini, tutajiuliza, tutajitazama, tutajipanga na kuweka mikakati ya usajili makini ili kuanzia msimu ujao tusiwe na hali ya kizungumkuti kama hii
    Tunaomba mashabiki wetu muendelee kutuunga mkono hasa wakati huu tunapoelekea kwenye mechi ngumu ya ligi kuu dhidi ya Ashanti United jumatano hii, Jumatatu Njema, Imetolewa na Utawala,”.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAOMBA RADHI KWA SOKA 'MBOFUMBOFU' NA MATOKEO MABAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top