• HABARI MPYA

    Monday, February 24, 2014

    ‘VIHIYO’ WAPIGWA KUMBO UCHAGUZI TASWA, KAMA HUJASOMEA UANDISHI WA HABARI HUNA SIFA ZA KUGOMBEA

    Na Dina Ismail, Dar es Salaam
    FOMU za wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam zimeanza kutolewa leo (Februari 24 mwaka huu).
    Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TASWA, 
    Boniface Wambura ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo zinazotolewa Idara ya Habari (Maelezo) ni Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.
    Vihiyo watatusamehe; Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TASWA amesema mtu ambaye hana cheti cha kitaaluma hataruhusiwa kugombea kwa mujibu wa Katiba, hilo ni pigo kwa waliovamia fani kutafuta urahisi wa maisha

    Amesema ada kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini na Mhazini Msaidizi ni sh. 50,000 kwa fomu. Nafasi za wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zinapatikana kwa sh. 20,000.
    Amesema kwa mujibu wa Ibara ya 21(e)(i), sifa ya elimu kwa wanaowania nafasi za Mwenyekiti hadi Katibu Msaidizi ni diploma au digrii ya uandishi wa habari. 
    “Kwa nafasi nyingine kwa mujibu wa Ibara ya 21(e)(ii) ni cheti cha ngazi yoyote katika uandishi wa habari. Tunawahimiza wanachama wa TASWA kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili waweze kuwania nafasi hizo,”amesema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ‘VIHIYO’ WAPIGWA KUMBO UCHAGUZI TASWA, KAMA HUJASOMEA UANDISHI WA HABARI HUNA SIFA ZA KUGOMBEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top