KOCHA David Moyes ametumia vikosi tofauti vya kwanza katika mechi zote 39 alizoiongoza Manchester United hadi sasa, lakini beki wa zamani wa Arsenal, Martin Keown ambaye kwa sasa anaandikia Daily Mail la Uingereza amempa ushauri wa bure.
Keown ameandika leo katika Daily Mail akimtaka Moyes kuacha kubadilisha vikosi na atumie kikosi cha kwanza kimoja tu, akiwaanzisha De Gea, Smalling, Evra, Valencia, Fletcher, Carrick, Mata, Rooney, Januzaj na Van Persie.
Man United imekuwa na mwenendo mbaya chini ya Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson aliyejiuzulu mwishoni mwa msimu uliopita na sasa inaelekea tu si kutema ubingwa, bali kukosa hata nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya mwakani.

Acha mapepe! David Moyes ameshauriwa kuacha kubadilisha vikosi Man United na atumie kikosi hicho hapo chini katika mechi zote.




.png)
0 comments:
Post a Comment