• HABARI MPYA

    Thursday, February 20, 2014

    ARSENAL HURUMA, YACHAPWA 2-0 NA BAYERN, OZIL AKOSA PENALTI, SZCZESNY ALIMWA NYEKUNDU

    BAYERN Munich imeendeleza ubabe wake, baada ya kuilaza Arsenal mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Emirates mjini London usiku huu katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Bao hilo pekee lililoizamisha Arsenal iliyomaliza pungufu ya mchezaji mmoja, lilipatikana dakika ya 54, mfungaji Toni Kroos aliyefumua shuti kali akiwa umbali wa mita 20 baada ya pasi ya Philipp Lahm.
    Picha hii inaonyesha namna Ozil alivyokosa penalti na Szczesny alivyopewa kadi nyekundu
    Pati la ushindi; Wachezaji wa Bayern wakimpongeza Kroos baada ya kufunga bao la kwanza Emirates usiku huu

    Thomas Muller akafunga bao la pili dakika ya 88 baada ya pasi nzuri ya Philipp Lahm tena.
    Arsenal ilipata pigo dakika ya 39 baada ya kipa wake Wojciech Szczesny kutolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kumuangusha winga wa Bayern Munich, Arjen Robben kwenye eneo la hatari.
    David Alaba akaenda kupiga penalti, lakini pamoja na kumpoteza maboya kipa Fabianksi akapiga nje mpira huo pembeni mwa nguzo ya lango chini.
    Mapema dakika ya nane, Arsenal walipoteza nafasi nzuri ya kupata bao, kufuatia Jerome Boateng kumkwatua hadi chini Mesut Ozil ndani ya boksi, lakini kiungo huyo Mjerumani akaenda kupiga penalti mbovu kabisa ikapanguliwa kiulaini na kipa Manuel.
    Penalti ya Ozil ilivyopanguliwa na chini rafu iliyoponza Szczesny kulimwa kadi nyekundu


    Kipa wa akiba Lukasz Fabianksi aliingia badala ya Cazorla akaenda kusimama langoni, na tangu hapo Arsenal wakalazimika kucheza mchezo wa kujihami.
    Katika mchezo mwingine usiku huu, bao pekee la Diego Costa dakika ya 83 limeipa Atletico ushindi wa 1-0 ugenini ya wenyeji AC Milan Uwanja wa Giuseppe Meazza.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL HURUMA, YACHAPWA 2-0 NA BAYERN, OZIL AKOSA PENALTI, SZCZESNY ALIMWA NYEKUNDU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top