• HABARI MPYA

    Friday, February 28, 2014

    MALINZI AWATIA KWENYE KAMATI MOJA RUGE MUTAHABA NA HOYCE TEMU

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati ya watu tisa kuratibu maadhimisho ya miaka 50 tangu TFF ilipojiunga na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
    TFF ilipata uanachama wa shirikisho hilo la kimataifa Oktoba 8, 1964 ambapo itaadhimisha miaka hiyo 50 kwa kufanya shughuli mbalimbali za mpira wa miguu.
    Hoyce Temu Mjumbe Kamati ya TFF

    Kamati hiyo itaongozwa na Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali, Gabriel Nderumaki wakati Katibu atakuwa Lina Kessy ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Soka ya Wanawake (TWFA).
    Wajumbe ni Ahmed Mgoyi, Hoyce Temu, Teddy Mapunda, Ruge Mutahaba, Richard Kasesela, Boniface Wambura na Meneja Biashara wa TFF anayetarajiwa kuajiriwa hivi karibuni.
    Kamati itafanya kikao chake cha kwanza Jumatatu (Machi 3 mwaka huu) kwenye hoteli ya Courtyard iliyopo Upanda Seaview saa 7 mchana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AWATIA KWENYE KAMATI MOJA RUGE MUTAHABA NA HOYCE TEMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top