• HABARI MPYA

    Thursday, February 27, 2014

    TWIGA STARS IMEIVA, SHEPOLOPOLO YATUA

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    WAKATI Zambia (Shepolopolo) imewasili leo mchana (Februari 27 mwaka huu), Twiga Stars imesema mazoezi yamewaingia barabara tayari kwa mechi dhidi ya Wazambia hao itakayochezwa kesho (Februari 28 mwaka huu).
    Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itafanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni, na hakutakuwa na kiingilio.
    Kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage

    Wakizungumzia mechi hiyo, Kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage na nahodha wa timu hiyo Sophia Mwasikili wamesema kikosi chao kimewiva kwa ajili ya mpambano huo baada ya kufanyia kazi upungufu uliojitokeza katika mechi ya kwanza.
    Twiga Stars ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14 mwaka huu jijini Lusaka kwa mabao 2-1, na inahitaji ushindi ili iweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika Oktoba mwaka huu nchini Namibia.
    Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Zambia katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv itacheza raundi ya mwisho na Zimbabwe.
    Msafara wa Shepolopolo una watu 26 ambapo wachezaji ni Anita Mulenga, Annie Kibanji, Carol Howes, Debora Chisanga, Emelda Musonda, Esther Mukwasa, Grace Zulu, Hazel Nali, Hellen Mubanga, Lweendo Chisamu, Meya Banda, Mirriam Katamanda, Misozi Zulu, Mupopo Kabange, Noria Sosala, Rachel Lungu na Susan Banda.
    Viongozi ni Maclean Daka, Charles Bwale, Kaluba Kangwa, Enala Phiri, Cornelia Chazura, James Nyimbili, Besa Chibwe, Dorothy Sampa na Kabungo Katongo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS IMEIVA, SHEPOLOPOLO YATUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top