WASHAMBULIAJI wa kimataifa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu mwezi uliopita wamecheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, klabu yao Tout Puissant Mazembe ya DRC ikikosa Kombe baada ya kufungwa jumla ya mabao 3-2 na CF Sfaxien ya Tunisia.
Ni msimu wa pili kwa wachezaji wote hao makinda tangu wajiunge na Mazembe, Samatta akitokea Simba SC na Ulimwengu akitokea Taasisi ya Soka Tanzania (TSA) na wakati huo huo akicheza kwa mkopo Moro United.
Ni ukweli usiopingika, klabu hiyo imesaidia mno kukuza viwango vya wachezaji hao kwa kuanzia kimchezo na hata kimaisha- sasa wanafurahia soka kwa sababu wamevuna matunda yake.
Lakini hatupaswi kusahau hawa ni wachezaji wenye uwezo mkubwa sana waliojaaliwa na mwenyezi Mungu wao na katika soka wanaweza kufanya makubwa zaidi ya waliyofanya Mazembe katika klabu za Ulaya.
Wanaweza kunufaika na kufurahia zaidi soka katika klabu za Ulaya- na wanaweza kuweka rekodi ambazo Watanzania wengi kwa sasa hatutarajii. Lakini hiyo ni endapo watakwenda sehemu nyingine, na si Mazembe.
Kwa miaka miwili ambayo wamekuwa Lubumbashi, wachezaji hao tayari wamekwishafanya yote na hakuna jipya linaloweza kutarajiwa tena kutoka kwao, zaidi kuanza kudumaa kama nyota wengine wa klabu hiyo akina Given Singuluma na Tressor Mputu.
Miaka mitatu iliyopita Mzambia Singuluma alikuwa ana ndoto za kucheza klabu kubwa Ulaya, lakini sasa anapigania namba tu ndani ya kikosi cha Mazembe- na kwa Samatta na Ulimwengu utegemee nini?
Siku zote mchezaji kama hapati changamoto mpya, lazima kiwango chake kitashuka na ataondoka haraka katika ramani ya soka, vivyo hivyo na kwa akina Samatta na Ulimwengu huu ni wakati mwafaka kwao kuondoka Mazembe na kusogea mbele.
Inafahamika sera ya mmiliki wa Mazembe, Gavana Moise Katumbi ni kutouza wachezaji wake wazuri na anawalipa vizuri kwa kiwango cha Afrika, lakini tujiulize sera hizo zinamsaidia nani?
Zaidi ni ubinfasi wake tu wa kutaka kukumbatia wachezaji nyota na wanaposhindwa kumpa mataji, anasajili wengine na waliokuwa tegemeo la timu wanahamia benchi, mwisho wake atawaacha.
Hivyo basi, ipo haja ya Katumbi kwanza yeye mwenyewe pamoja na fedha zake kueleweshwa umuhimu wa kuruhusu vijana wakasogea mbele mapema katika umri mdogo kwenda kujitafutia maisha.
Niliwahi kungumza na Samatta akawa anasikitikia kitendo chake cha kusaini Mkataba wa muda mrefu na Mazembe, miaka minne akitokea Simba na akasema hiyo ni kwa sababu wakati huo alikuwa ana kiu tu ya kutoka nje, hakutaka kutazama kingine.
Lakini pia Samatta aliniambia, akisoma habari wachezaji fulani fulani wanalipwa fedha kadhaa kwa wiki Ulaya na akatathmini uwezo wao akilinganisha na wake, roho inamuuma sana kwa sababu anaamini anawazidi.
Kwa Mkataba aliosaini Samatta na Mazembe ina maana atakuwa tayari kuondoka Lubumbashi akiwa ana umri wa miaka 25, akacheze wapi Ulaya? Huu ndiyo wakati wake akiwa ana umri wa miaka 22 na uwezo wake upo juu, rekodi yake imekaa vizuri kuanzia klabu na timu ya taifa, ‘Poppa’ anauzika.
Wenzetu Kenya na Uganda huwa wanawapigania wachezaji wao kuhakikisha wanakuwa katika mazingira mazuri, ili waweze kuzisaidia timu za taifa baadaye kuzijengea heshima nchi zao- lakini Tanzania bado hatujawa na utamaduni huo, ila wakati umefika sasa tuwaige jirani zetu.
Yale mamilioni tunayotoa kutangaza utalii wetu Ulaya na Amerika tungeyanusuru kama tungekuwa na wachezaji japo wawili wanaocheza klabu zenye kufahamika Ulaya.
Uganda kama wasingesimama kidete kupambana dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia, leo hii Emmanuel Okwi angekuwa bado hachezi- lakini si hivyo tu unaweza kuuona mkono wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) nyuma ya mafanikio ya wachezaji kama Dennis Oliech, McDonald Mariga na Victor Wanyama.
Suala la Samatta na Ulimwengu kuondoka Mazembe wakati huu si jepesi, lakini ni muhimu sana na wao peke yao hawawezi kumshawishi bilionea mwenye jeuri ya fedha aliyezitakatalia klabu kibao za Ulaya kuziuzia wachezaji. Tunawasaidiaje? Mimi na wewe kama wadau wa soka, mamlaka za soka na serikali yetu chini ya rais mpenda michezo, Jakaya Kikwete tujiulize. Jumatano njema.

.png)
0 comments:
Post a Comment