• HABARI MPYA

    Sunday, December 15, 2013

    SIMBA SC YAWACHAPA KMKM 3-1 TAIFA BERKO LANGONI

    Na Mahmoud Zubeiry, Temeke
    SIMBA SC imeifunga KMKM ya Zanzibar mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Said Ndemla dakika ya 11 na Edward Christopher dakika ya 16.
    Kipindi cha pili, KMKM walibadilika na kuanza kupeleka mashambulizi langoni mwa Simba SC wakionana kwa pasi nzuri, ingawa pia Wekundu wa Msimbazi nao waliendelea kushambulia.
    Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la pili lililofungwa na Edward Christopher wa pili kushoto leo Uwanja wa Taifa 

    KMKM ilipata bao lake la kufutia machozi dakika ya 71, mfungaji Ally Ahmed ‘Shiboli’ kwa penalti, baada ya beki wa Simba kumchezea rafu mchezaji huyo. 
    Baada ya bao hilo, Simba SC ikiongozwa na Uhuru Suleiman katika safu ya ushambuliaji iliongeza kasi ya mashambulizi kusaka mabao zaidi.
    Juhudi hizo zilizaa matunda dakika ya 89, baada ya Henry Joseph kufunga kwa penalti kufuatia mchezaji mmoja wa Simba kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari.
    Matokeo haya yanamanisha kocha mpya wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic ameanza vyema kazi, hii ikiwa mechi yake ya kwanza tangu aanze kuifundisha timu hiyo.   
    Said Ndemla ashangilia bao lake na chini ni Edward Christopher akishangilia bao lake
    Baada ya mchezo huo, Simba SC itashuka tena dimbani Desemba 21, kumenyana na mahasimu wao wa jadi, Yanga SC katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, ulioandaliwa na wadhamini wa timu hiyo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Yaw Berko, Haruna Shamte, Omary Salum, Henry Joseph, Joseph Owino, Jonas Mkude, Uhuru Seleiman, Said Ndemla/Ramadhan Kipalamoto dk76, Edward Christopher/William Lucian dk40, Betram Mwombeki/Tambwe dk30/Issa Abdallah dk86 na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
    KMKM; Mudathir Khamis, Kassim Nemshi, Faki Ali, Khamis Ali, Iddi Mgeni/mudrik abdallah, Ibrahim Khamis/makame nuhu, Nassor Ally, Juma Mbwana, Hadji Simba, Ali Ahmed ‘Shiboli’ na Maulid Kapenta/Khalid khamis.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAWACHAPA KMKM 3-1 TAIFA BERKO LANGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top