• HABARI MPYA

    Thursday, December 26, 2013

    MAN UNITED YAIPIGA 3-2 HULL CITY, ARSENAL NA CHELSEA NAZO ZASHINDA

    KLABU ya Manchester United imetoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda 3-2 dhidi ya Hull City Uwanja wa KC, huku mchezaji wa zamani wa Mashetani hao Wekundu James Chester akijifunga kuamua mshindi.
    Chester alitangulia kuifungia Hull dakika ya nne, Meyler akafunga la pili dakika ya tatu na Man United ikazinduka na kupata bao la kwanza dakika ya 19 kupitia kwa Smalling, pasi ya Rooney aliyefunga la kusawazisha dakika ya 26.
    Man United ilijihakikishia pointi tatu dakika ya 66 baada ya Chester kujifunga. Katika mchezo mwingine, bao pekee la Edin Hazard dakika ya 29 liliiipa ushindi wa 1-0 Chelsea dhidi ya Swansea Uwanja wa Stamford Bridge.
    Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham United Uwanja wa Boleyn, mabao ya Theo Walcott dakika ya 68 na 71 na Lukas Podolski dakika ya 69. Bao pekee la West Ham limefungwa na Cole dakika ya 46.
    Aston Villa imefungwa 1-0 na Crystal Palace, Cardiff City imefungwa 3-0 na Southampton, Everton imefungwa 1-0 nna Sunderland, Newcastle United imeifumua 5 - 1 Stoke City, Norwich City imefungwa 2-1 na Fulham na Tottenham Hotspur imetoka sare ya 1 - 1 na West Bromwich.

    Time to celebrate: Man United have moved to within five points of leaders Liverpool having played a game more
    All white on the night: The own goal came from Ashley Young's cross midway through the second half
    All white on the night: The own goal came from Ashley Young's cross midway through the second half
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YAIPIGA 3-2 HULL CITY, ARSENAL NA CHELSEA NAZO ZASHINDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top