Na Mahmoud Zubeiry, Nakuru
MSHAMBULIAJI mpya wa Simba SC, Ali Badru amemaliza mechi za makundi ya
Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mjini hapa bila
ya kufunga bao hata moja.
Kocha Salum Bausi alimuanzisha Badru katika mechi zote mbili za kwanza za
Kundi A dhidi ya Sudan Kusini na Ethiopia, lakini baada ya kushindwa kufunga
akamuanzishia benchi katika mechi ya jana na Kenya.
![]() |
| Badru hajafunga bao hadi sasa Challenge |
Bausi alilazimika kumuingiza Badru dakika ya 51 kuchukua nafasi ya Khamis
Mcha ‘Vialli’ wa Azam FC, ambaye naye pia amecheza mechi mbili za makundi bila
kufunga.
Hata hivyo, mshambuliaji huyo aliyesajiliwa Simba SC kutoka Canal Suez ya
Misri alishindwa kuinusuru Zanzibar na kipigo cha 2-0 kutoka kwa wenyeji
Harambee Stars.
Angalau kiungo mpya wa Wekundu hao wa Msimbazi, Awadh Juma Issa
aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar, alifunga bao zuri la kufutia machozi dhidi
ya Ethiopia, Zanzibar ikilala 3-1.
Kiraka wa Wekundu hao wa Msimbazi, Adeyum Saleh alifunga bao katika ushindi
wa 2-1 dhidi ya Sudan Kusini, wakati bao lingine la Zanzibar siku hiyo
lilifungwa na kiungo wa Coastal Union, Suleiman Kassim ‘Selembe’.



.png)
0 comments:
Post a Comment