• HABARI MPYA

    Monday, December 02, 2013

    NIYONZIMA MAJANGA CHALLENGE, RWANDA YALAMBWA TENA KIDUDUE NA SUDAN

    Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
    BAO pekee la Salah Ibrahim dakika ya 29, limeipa ushindi wa 1-0 Sudan dhidi ya Rwanda katika mechi ya Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Uwanja wa nyasi bandia wa City, Nairobi.
    Kipigo hicho kinaiweka Rwanda katika mazingira magumu ya kusonga Robo Fainali, baada ya awali pia kufungwa na Uganda 1-0 katika mchezo wao wa kwanza.
    Mshambuliaji wa Rwanda, Ndahinduka Michale akitafuta mbinu za kumgeuza beki wa Sudan, Elrayah Ali Maki katika mchezo wa leo Uwanja wa City

    Nahodha wa Rwanda, Haruna Niyonzima anayechezea Yanga SC ya Dar es Salaam alijitahidi mno kuwatengenezea nafasi washambuliaji wake, Meddie Kagere na Ndahinduka Michale, lakini walishindwa kuzitumia.
    Mchezo wa pili wa Kundi C baina ya Uganda na Eritrea ndiyo unaanza muda huU Uwanja wa City. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIYONZIMA MAJANGA CHALLENGE, RWANDA YALAMBWA TENA KIDUDUE NA SUDAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top