• HABARI MPYA

    Monday, December 02, 2013

    OKWI, KIIZA WAIPELEKA UGANDA ROBO FAINALI CHALLENGE

    Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
    MABINGWA watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika Masharik na Kati, CECAFA Challenge, Uganda The Cranes wamejihakikishia kutinga Robo Fainali ya michuano ya mwaka huu baada ya kuifunga Eritrea mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi C, Uwanja wa City, Nairobi, Kenya.
    Mabao ya Cranes leo yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Emmanuel Arnold Okwi mawili dakika za tisa na 39 na mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Friday Kiiza kwa penalti dakika ya 19. 
    Emmanuel Okwi ameifungia mabao mawili Uganda leo

    Ushindi huo, unaifanya Uganda itimize pointi sita baada ya awali kushinda 1-0 dhidi ya Rwanda na kupanda kileleni mwa Kundi hilo kwa wastani wa mabao, kwani hata Sudan ina pointi sita.
    Hali mbaya kwa Rwanda baada ya kufungwa mechi ya pili leo 1-0 na Sudan, mustakabali wao wa kutinga Robo Fainali upo katika nafasi mbili za ‘best loosers’.
    Dan Sserunkuma hapa alichezewa rafu iliyosababisha penalti, Hamisi Kiiza akafunga. Chini Kiiza na Okwi wakishangilia bao la pili la The Cranes

    Katika Kundi A, wenyeji Kenya na Ethiopia wapo katika nafasi nzuri za kwenda Robo Fainali na Zanzibar inayoshika nafasi ya tatu, inaweza kuangukia katika kuwania moja ya nafasi mbili za best losers. Lakini iwapo Zanzibar itaifunga Kenya, wenyeji hao nao watawania Robo Fainali katika nafasi mbili za best loosers.
    Kundi B Zambia imejihakikishia kwenda Robo Fainali na mechi baina ya Tanzania Bara na Burundi itaamua timu ya kuungana na mabingwa hao wa zamani wa Afrika na ya kuwania kufuzu kwa nafasi za best losers.      
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI, KIIZA WAIPELEKA UGANDA ROBO FAINALI CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top