| Mshambuliaji wa Yanga SC, Mrisho Ngassa kushoto akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu yake, Abdallah Ahmed Bin Kleb kulia Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jana jioni. Ngassa alikuwa amewasili na kikosi cha Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' kutoka Nairobi, Kenya walipokuwa wakishiriki Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge wakati Bin Kleb na viongozi wenzake kadhaa, walijitokeza kuwalaki wachezaji hao. |
0 comments:
Post a Comment