IMEWEKWA AGOSTI 18, 2013 SAA 2:35 USIKU
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amesherehekea kurejea kwake Stamford Bridge kwa kuanza na ushindi wa mabao 2-0 katika Ligi Kuu ya England dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu, Hull.
Kiasi cha miaka sita tangu aachane The Blues, kocha huyo maarufu kama Special One alifurahia mapokenzi mazuri na mchezo mzuri wa timu yake akirejea nyumbani.
Haikuwa kazi rahisi kwa Chelsea kushinda, baada ya mkwaju wa penalti wa Frank Lampard dakika ya sita kuokolewa na Allan McGregor na sheria ya teknolojia kwenye mstari wa goli ikachukua nafasi yake wakati kipa huyo wa Scotland alipookoa mpira wa kichwa wa Branislav Ivanovic na kudhaniwa ni bao dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza, ikisahihisha si bao.
Pamoja na hayo, Chelsea ilipata mabao yake yote kipindi cha kwanza kupitia kwa Oscar dakika ya 13 na Lampard dakika ya 25.
Kikosi cha Chelsea leo kilikuwa: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Lampard, Ramires, De Bruyne/Schurrle dk67, Oscar/van Ginkel dk85, Hazard, Torres na Lukaku dk75.
Hull City: McGregor, Elmohamady, Chester, Davies, Figueroa, Brady, Meyler/Huddlestone dk59, Koren, Sagbo, Graham/Livermore dk59 na Aluko/Boyd dk79.

Amerudi: Jose Mourinho akiuonyesha ishara ya busu umati Uwanja wa Stamford Bridge katika kurejea kwake

Shwari kabisa: Oscar akishangilia na Torres baada ya kufunga

Rahisi namna hii: Oscar akishangilia

Allan McGregor akijaribu kupangua dhidi ya Fernando Torres

Anakosa: Frank Lampard alishuhudia mkwaju wake wa penalti ukiokolewa na McGregor

Anasahihisha makosa: Lampard alisahihisha makosa yake kwa kufunga kwa mpira wa adhabu muda mfupi baada ya kukosa penalti


Pasi saba: Chelsea ilifanya shambulizi la haraka kuibomoa ngome ya Hull kabla ya Oscar kufunga

Amezuia: McGregor akizuia mpira wa kichwa wa Branislav Ivanovic

Si bao: GDS imesema mpira wa Ivanovic haukuvuka mstari

Furaha: Mashabiki Chelsea wakionyesha kumuunga mkono Mourinho



John Terry alisumbuliwa mno na mchezaji mpya wa Hull, Yannick Sagbo

Kifaa kipya: Kevin De Bruyne alivutia akianza kazi The Blues

Torres akipambana


.png)