IMEWEKWA AGOSTI 11, 2013 SAA 1:11 USIKU
MABAO ya Romelu Lukaku na kiungo mkongwe, Frank Lampard yameipa Chelsea ushindi wa 2-1 dhidi ya AS Roma katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu mjini Washington.
Kiungo huyo alifunga bao kwa shuti la mbali ambalo lilikuwa la kusawazisha dakika ya 60, baada ya Eric Lamela kutangulia kuifungia Roma dakika ya 20.
Romelu Lukaku akaendelea kumpa raha kocha Jose Mourinho, baada ya kufunga bao la dakika ya 89.
Katika mchezo wa huo, kikosi cha Chelsea kilikuwa: Schwarzer/Blackman dk46, Azpilicueta/Ivanovic dk57, Luiz/Cahill dk46, Terry/Lukaku dk78, Bertrand, Mikel/Van Ginkel dk57, Essien/Lampard dk46, Moses/Ramires dk46, De Bruyne/Oscar dk46, Schurrle/Hazard dk57 na Torres/Ba dk46.
Roma: De Sanctis; Maicon/Jedvaj dk78, Benatia, Castan, Balzaretti; Bradley, Strootman, Florenzi/Marquinho dk69, Lamela, Osvaldo/Borriello dk69 na Totti/Tallo dk85.

Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga

Mchezaji wa Roma, Erik Lamela akiifungia timu yake bao la kuongoza kufuatia makosa ya kipa Mark Schwarzer

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akisalimiana na kipa wa Roma, Morgan de Sanctis

Beki wa Roma, Mehdi Benatia (kushoto) akipambana na kiungo wa Chelsea, Eden Hazard

La ushindi: Morgan de Sanctis akishuhudia mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku ukitinga nyavuni

Lukaku akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la ushindi


.png)